PF imeweza Zambia, CHADEMA tujiandae kuondoa kinga kwa Marais wastaafu baada ya 2015

Ben Saanane

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2007
Posts
14,580
Reaction score
18,230
Note:Moderators msiiunganishe hii,Tutaikumbuka Mungu akipenda baada ya uchaguzi mkuu 2015 kama tutakua hai.

Kinga za Marais wa zamani Jakaya kikwete na Benjamin Mkapa zitakapoondolewa mwaka 2015 baada ya CHADEMA kuingia ikulu itakua fundisho kwa watawala wa muda huo na baadae.Bunge la Zambia lilimuondolea Rais wa Zamani Rupiah Banda kinga ya kutoshtakiwa ijumaa iliyopita.Leo Rupiah Banda amekamatwa na atashtakiwa kwa makosa ya ufisadi,matumizi mabaya ya madaraka na kutumia mabilioni ya hela kutoka hazina kufadhili kampeni za uchaguzi mkuu kama CCM walivyofanya kupitia EPA mwaka 2005.Pia anatuhumiwa kuliingizia taifa hasara kubwa kutokana na mkataba wa ununuzi wa nishati ya mafuta kama ilivyokua kwa Mkataba tata wa RICHMOND hapa Tanzania.

Watoto wa rupiah banda walishtakiwa kwa tuhuma za kujinufaisha na tenda za serikali kinyume na taratibu.Watoto wa wa watawala wana cha kujifunza kutoka kwa Willium Banda na kaka zake.

Rupiah Banda anatoka chama tawala cha zamani cha UMD(CCM ya Zambia).Chama tawala cha sasa Patriotic Front (PF)kilikua chama kikuu cha upinzani kilichoshabihiana karibia kila kitu na (CHADEMA) na hatimaye kikashinda kampeni chafu na propaganda za udini na ukabila mwaka 2011 na kuingia ikulu ambapo Michael Satta(Mwenye msimamo mkali dhidi ya ufisadi kama Dr.Slaa) aliunda serikali.Aliahidi kuisafisha ikulu kama alivyoahidi Dr.Slaa mwaka 2010 kwenye kampeni.Watanzania tuna cha kujifunza na tujiandae/wajiandae kisaikolojia.

Honestly,I weep for my country. Until we are able to stand up and say enough is enough, this madness will continue in Tanzania, where corrupt politicians will plunder our national wealth and destroy the future of our Children.
Tanzanians, why do we watch while our country is a laughing stock in the international community? Tell me which country, business entity or investor that will take Tanzania serious after this shame brought to us by looters? Tujiandae kupiga hatua hii muhimu kwa maandalizi ya kuondoa CCM turudishe heshima ya ikulu.

(pichani wafuasi wa michael satta kampeni za mwaka 2011,Basi hilo ni mojawapo wa vitendea kazi vilivyonunuliwa na fedha kutoka hazina-EPA ya Zambia)


-EPA ya Zambia)


Hapa chini Michael Sata wa chama cha upinzani akihutubia kwenye kampeni ambazo vijana wengi walijiandikisha kupiga kura.Aliwahakikishia kuwa ataisafisha ikulu.Waliiamini kauli hiyo kuliko propaganda za udini na ukabila za MMD(CCM ya Zambia)



Baada ya tume ya uchaguzi kutangaza matokeo.Vijana wa Zambia hapa chini walimiminika mtaani kufurahia kwamba ikulu inakwenda kusafishwa



(Pichani hapo chini Michael Satta) akiapa.
 
Watanzania kama tumelogwa. Hata Kenya tunawashutumu kwa ukabila lkn waliweza kumwandoa Moi na Kanu yake. Hapa watakuja watu ambao akili zao haziwezi kuona kuwa tunahitaji mabadiliko kwa sababu wanafaidi na mfumo mbovu tulionao.

Be it through Chadema, CUF, NCCR or TLP, CCM must go.
 
Siasa za Copy & Paste as usual, Tanzanian style, kwa hiyo na mimi nimeamua kufanya hivyo kwa hii article chini kubeba mifano uliyoileta ya watu wajiandae kisaikologia
By the way, kwa nini tu iwe kwa Rais Mkapa na Rais Kikwete na isiwe kwa Mwalimu Nyerere au Rais Mwinyi. Is this witch-hunt at it's best?.

Ni angalizo tu, wala hakuna umaana wowote wa kulijibu.
 

Hiyo article unategemea Amsterdam aandike tofauti na hiyo?

What do you mean kuwa 'Witch-hunt'?

Tukiwa na katiba nzuri ambayo inacheck intergrity ya Rais huku Bunge na Mahakama likiwa independent na kuwa na uwezo wa kui-check exeacutive kutakua hakuna haja ya kumuondolea rais kinga tena.Sasa hivyo vyote havikuwepo Zambia na hata Tanzania kwa muda huu kinachowafanya Marais kuwa wazembe kutumia madaraka vibaya.Kwa hiyo watawala wanajifanyia mambo ya ovyo tu.

Bunge lingekua na uwezo wa kufanya check and balance kwamadudu ambayo wamefanya si ajabu impeachment ingefanyika na bunge hivyo wala tusingesubiri amalize muda wake ashtakiwe.Ni kama ilivyokua kwa akina Richard Nixon Marekani na Gerald Ford kwenye kashfa ya WATERGATE.Kwa hiyo ili heshima ya Rais mstaafu iwepo na kinga yake basi tukubali kuwa na separation of power kwa ajili ya check and balance

Unasema tunaiga,mbona husemi hata mfumo wa kisiasa na demokrasia ya magharibi tumeiga?
 
Baada ya kutoka Kenya mkaangukia pua sasa mmeamua kwenda kujifariji na kujiliwaza kwenye siasa za Zambia.

Kwanza Zambia hakuna udini unaouzungumzia 80% ni Wakiristo.

Michael Satta wa PF kasaidiwa na Kanisa mpaka kuchukuwa madaraka hapa umekwepa kumfananisha na Dr Slaa sijui umehofia nini.

Huwezi kufananisha siasa za Zambia na Tanzania.

Chadema hawana sifa ya kuiongoza Tanzania.
 

Mkuu ulichokiandika hapo ni ukweli mtupu usiokuwa na chenga;

Napenda kuto mchango wangu kuhusiana na mashabiki wa chama TWAWALA (CCM); ukubali ukatae Shabiki awaye yeyote wa CCM ataangukia mojawapo ya makundi haya katika jamii yetu;

Group la kwanza linajumuisha watu ambao either wao wenyewe ni mafisadi au watoto wao, ndugu zao, jamaa zao na rafiki zao wananufaika na fedha za ki-fisadi zinazotokana na mfumo dhalimu uliopo.

Group la pili linajumuisha watanzania ambao hawana habari juu ya nini kinacho endelea nchini mwetu na duniani kwa ujumla; Lakini nachelea kusema hili group members wake ni wachache sana kwani hata vijijini watu wanafuatilia kwa ukaribu sana na kuchambua habari vilivyo.

Group la tatu linajumuisha wananchi ambao either akili zao zinategea au ni machizi; na ndiyo maana hapa mtaani kwetu mashabiki wote wa CCM kwa ujumla wao wanajulikana kwa jina maarufu la MISUKULE kwani tuna amini ni wale ambao akili zao zimewekwa mateka.

Group la mwisho linajumuisha maofisa waandamizi wa serikali ambao nafsi zao zinaichukia CCM na mfumo wake, huku wakiendelea kuipigia debe hadharani either kwa ajili ya maslahi yao binafsi au kwa ajili ya kunusuru maisha yao, ili uhai wao usije ukakatishwa kama akina Kolimba.
 
Aboud Jumbe naye anakinga? Dr Ritz hebu nisaidie.
 
Swadacta, ndio ilivyo 100%, hakuna ila!
 

Mkuu usikurupuke soma kwanza post ya Kamanda Ben Sanane ukisha ielewa ndo uanze kuchangia na endapo hujaielewa omba msaada usaidiwe, siyo kujifanya kila kitu unajua.

Mkuu endapo Jakaya Mrisho Kikwete ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, am telling you hata TEJA anaweza kuwa Rais wa Tanzania.
 
CCM wanajua hili ndo maaana wapo tayari kwa hila,ghiliba,vurugu na kila kitu kilico ndani ya uwezo wao kutoruhusu hicho kitokee Tanzania,hatujaona kitu bado watakuja na kali zaidi ya hizi tunazoziona.
 

Dr Slaa kafananishwa Satta, PF imefananishwa na Chadema.

Tatizo lenu nyie Pro-Chadema wote ni mateka wa Chadema.

Kuna kitu gani cha ajabu kimeandikwa mpaka mtu aombe msaada.
 
THANK YOU VERY MUCH!!.
Mkuu, Kumbe Mzizi wa Tatizo unaufahamu vizuri. Kwa sababu kumuondolea kinga Rais hakuondowi tatizo kama ilivyojidhihirisha Zambia, kwani si hata kwa Chiluba waliondoa na wakamshitaki. what happened baada ya hao wengine kuingia madarakani. They did the same Chiluba alivyofanya kwa sababu bunge lilikuwa overlooked.

Yes, Rais ni taasisi inayoongozwa na watu kama mimi, ambao tuna mapungufu. kunahitajika check and balance kama unavyosema katika utendaji.

Tatizo ndiyo hilo, na nchi kwa sasa iko kwenye mchakato wa katiba mpya. Ni tumaini la kila mpenda nchi kupata katika ambayo itakuwa mwarobaini wa matatizo kama haya (iwapo yapo) lakini siyo viongozi wa vyama vya siasa kama unavyotaka kuniamisha.

Mkuu, jaribu kutojenga hoja ya kitaifa kwa macho ya chama chako kama ndiyo mwarobaini wa matatizo ya nchi na kwa kutumia mifano ambayo ni hafifu kama huu wa Zambia.
 

Sasa hata kama tutakua na katiba mpya haitazuia watu kuwajibika kwa madhambi yao.Ni lazima tuachane na impunity ili iwe fundisho.Wakati huo huo tuzingatie haya uliyoandika na nilichoandika hapo juu kuhusu check and Balance
 
Dr Slaa kafananishwa Satta, PF imefananishwa na Chadema.

Tatizo lenu nyie Pro-Chadema wote ni mateka wa Chadema.

Kuna kitu gani cha ajabu kimeandikwa mpaka mtu aombe msaada.

Mkuu ni dhahiri familia yenu nzima mnamwogopa sana huyo mzee pamoja na Dola yenu, kwani yupo straight forward na huwa hamumunyi maneno; Alisha tamka "Waacheni waendelee kujenga mahotel yao huko mbugani na kwingineko, kwani tukisha kamata dola hizo zote ni mali za serikali".

Vipi kijiji cha Birila-Kempisk kilichopo Serengeti ujenzi wake umesha kamili au ndo upo kwenye finishing?
 
Sasa hata kama tutakua na katiba mpya haitazuia watu kuwajibika kwa madhambi yao.Ni lazima tuachane na impunity ili iwe fundisho.Wakati huo huo tuzingatie haya uliyoandika na nilichoandika hapo juu kuhusu check and Balance
Mkuu, Hekima na busara katika siasa kwa Africa ni tunu ambayo Mungu amewapa wanasiasa wachache sana kama Mandela.

Mandela pamoja na kupata lungu la madaraka, aliamua kuanza ukurasa mpya kwa kiyasahau yaliyopita pamoja na kwamba yeye alikuwa pia ni muathirika sana na siasa za kibaguzi. Hakutaka kulipiza kisasi kwa kutambua kuwa historia imebainisha, pale unapolipiza kisasi, hicho kisasi kitakuja tena kulipizwa kwako, kwa maana kuwa, nchi inakuwa inaongozwa kwa misingi ya with-hunt kama inavyotokea Zambia.

Kuna njia nyingi za kutoa fundisho la kisiasa kwa wanasiasa. Mandela alitoa fundisho la kisiasa ambalo ni wachache sana waliamini kama kuna fundisho la aina hiyo.

Matatizo ya Tanzania hayakuanzia katika utawala wa Rais Mkapa na yataishia kwa Rais Kiwete. matatizo ya Tanzania yameanza toka nchi ilipopata uhuru. Kama ni kutoa fundisho unalotaka, usifanye cherry picking. Anzia kwa Mwalimu Nyerere na endelea mpaka whatever lakini ukumbuke, historia ya visasi itakushitaki mbeleni kama inavyotokea Zambia.
 
Patriotic Front (PF)kilikua chama kikuu cha upinzani kilichoshabihiana karibia kila kitu na (CHADEMA)

Mkuu waweza fafanua. Maana siku hizi Chadema kinakuwa compared na kila mtu. Wiki iliyopita kuna mtu alileta uzi eti Chadema kama Mandela na watu walivyo kondoo (bendera fuata upepo) wote wakasema ndiyoooo.
 
Wa Tanzania wataishia kuendelea wakiangamia kwa ujinga wao wenyewe. Ni watu wajinga wasioona umuhimu wa kujipigania iliyo haki yao. Ni Mazezeta wenye nidhamu ya woga na na watu waliokosa utashi wa kudhubutu hata kwa jambo ambalo litaboresha maisha yao na kizazi cha watoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…