Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Utaratibu wa kuchukua PF3 FORM kwanza kituo cha POLISI na ndipo upeleke mgonjwa hospital ambaye kila Sekunde inayogonga ni muhimu sana kuokoa maisha yake, imapitwa na wakati.
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Ngosha wetu Kanumba (RIP) angeliweza kupona kama si uzembe fulani wa kucheleweshwa kufika hospital na ndiyo hiyo form PF3 ianze kutafutwa.
Ombi kwangu kwa ndugu Tundu Lissu ambaye najua akijipanga vizuri kwa hili, anaweza kuliteka Bunge letu na hii sheria ikabadilika.
Ombi kwa Waziri wa Sheria, waziri wa mambo ya ndani ambao nao kama kweli wameguswa na kifo cha Kanumba, basi watumie muda huu kufikiri utaratibu wa kubadilisha hii sheria ambao imeshapoteza maisha ya wengi na itaendelea kupotea.
Ombo kwenu Wabunge wote mnaoingia Bungeni leo hii, kukaa na kujadili na hadi mwisho kupitisha utaratibu mpya wa huduma ya kwanza na ikibidi kama haipo sheria basi iwekwe kuwa "ni lazima kutoa msaada kwa majeruhi." Usipotoa msaada hata kama ni kuita jirani au kuita ambulance, basi uhukumiwe.
Mwisho kwa wadau wote wa Sheria na Watanzania kwa ujumla, tumeshaona kuwa PF3 form inapoteza muda mwingi sana wa majeruhi kufika hospital, muda ufike sasa huu utaratibu ubadilike. Tulipigie kelele hili swala kwa wabunge wetu popote wanapopita.
Kwa Wabunge waliopo hapa JF kama Homeboy Kigwangallah, Nchemba Mwigulu, Zitto, Mnyika, Mo, na wengine mliojificha kwenye NICKNAME, Waziri Mkuu na Rais ambao nafahamu mnapita humu ndani, tafadhali sana tunaomba huu utaratibu MUUBADILISHE. Huduma ya kwanza iwe namba moja na ndiyo form ya PF3 ije.

Naomba kuuliza mtu akipata majeraha anatibiwa hospitali au mpaka ende na fomu ya polisi? (PF3?)
Mpaka PF3 form, sijui kama kuna exceptions Ila kwa uelewa wangu ni hivyo.
.....na huu ni uzembe uliopitiliza ila watendaji wameufumbia macho.
Kwenye 'ajali' every minute counts...
Internal injuries, kwa kitaalamu hauruhusiwi kumsogeza mgonjwa kwa namna yoyote
kuepusha irreversible damages... Unless mgonjwa atakuwa anahudumiwa na qualified 1st Aider, au
unamsaidia under instruction toka kwa mtaalamu..
kwa nchi za wenzetu ukijipendekeza kumgeuza majeruhi waweza jikuta kizimbani...
bht hakuna ni ujinga fulani tu, hili swala lilijadiliwa sana bungeni miaka ya 90 mwanzoni lakini wapi...PF3 liko tu!
ilitakiwa mtu anapatiwa huduma, hospitali wanatoa taarifa polisi, wakati anapatiwa huduma ..polisi wanakuja pale kuchukua taarifa kama majeraha ni criminal cases au la
Walitakiwa waziamuru hospitali kutowatoa wagonjwa baada ya kupatiwa tiba kama kuna dalili ya ugongwa kusababishwa na kudhuriwa.
Sio hii mtu mahtuti kwanza ikasakwe PF3
Point...
Maana kama relevance ni kutaka kumchukulia hatua za kisheria muhusika hiyo ingekuwa njia mbadala tu na ambayo haihatarishi maisha ya mdhurika....
Mtu unamaumivu upite kituo cha polisi, waanze kutafuta karatazi na kalamu ziko wapi...nani asiyejua sharau za wenzetu hawa, hawana sense of agency wao, waanze kuwarushia na maneno, mtu anaangamia tu hapo.
Watunga sheria wenyewe ndo hao hawana hoja wana viroja tu...
Vichwani watupu...
Wabinafsi na wasiojali hata kilichowapeleka huko bungeni...
Sheria zetu nyingi ni mbovu kupita maelezea na sijui inahitaji karne ngapi ili waelewe maHitaji yetu na kuyafanyia kazi!