SoC04 PF3 na pesa zisiwe Mbele ya uhai wa mtu. Uhai wa raia ni Bora kuliko "makaratasi"

SoC04 PF3 na pesa zisiwe Mbele ya uhai wa mtu. Uhai wa raia ni Bora kuliko "makaratasi"

Tanzania Tuitakayo competition threads

FravoB

Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
22
Reaction score
59
Naandika maneno haya nikiwa kwenye maumivu makali Sana. Nimempoteza mtu wa muhimu sababu ya PF3.
PF3 Ni kiungo gani kwenye afya ya binadamu!!??

Natamani makala yangu isomwe na nchi nzima Kisha mnisahihishe pale ninapokosea, huenda Ni maumivu ndo yanaandika haya, Ila Hata niandikaje Hawezi amka Tena.

Tanzania tuitakayo ina malengo mengi sana, Ila katika hayo mengi la afya liwe la kwanza. Tunapoteza ndugu zetu na nguvu kazi kwa sababu ya Sheria za maana, Ila hizi Sheria tunaomba zituhurumie.

Mgonjwa amepata ajali, anafika hospital hapatiwi matibabu sababu ya PF3.

Aliyefika na unafuu anazidiwa mbele ya wahudumu hawampatii matibabu sababu ya PF3.

Aliyefika amezidiwa baada ya kupata ajali mpaka umauti unamfika bila kupatiwa matibabu sababu ya PF3.

Naomba niulize tena PF3 Ni kiungo gani kwenye afya ya binadamu!!?

Tunatambua umuhimu wa PF3 kwa mtu aliyepata ajali pale anapohitaji matibabu. Hivyo kwa kutii Sheria zilizowekwa wahusika huwa wanawajibika kwa usahihi.

Ombi langu kwenye sekta ya afya. Mbinu mbadala itafutwe ili kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wameshindwa kupata PF3 kwa wakati kwani afya Ni Bora kuliko makaratasi.

Tunapoteza ndugu na watu wa muhimu ambao ni nguvu kazi ya Taifa, na ni sehemu ya maendeleo katika jamii yetu kwa sababu ya PF3.

Naomba niulize tena, PF3 Ni kiungo gani kwenye afya ya binadamu!!?.
1719356245899.jpg

Chanzo: Jamii forums Online.

Tanzania tuitakayo inajengwa kwa nguvu kazi na mshikamano na ushirikiano, Je! mtu mmoja anapopungua katika nguvu kazi haitaleta madhara. Je! raia mmoja anapopungua katika nguvu kazi ya kulijenga Taifa haitaleta hasara kwa miaka 5, 10 na 25 ijayo.

Tuchukue mfano hai kwa wachina kipindi Cha Vita yao na wajapani, kupitia sinema zao wanazoigiza huwa tunaona mchina akipoteza mwanajeshi mmoja kwake ni hasara kubwa Sana na maumivu yake ni makubwa, lakini mjapani akipoteza wanajeshi wengi haaoneshwi kuumizwa sawa na mchina. Na mwisho wa vita mchina anashinda Vita Ile yote Ni kwa sababu aliwapa vipaumbele watu wake hivyo Hata umakini wa kuwalinda unaongezeka.

Sijamaanisha kwamba nchi ya Tanzania haitoi vipaumbele kwa wananchi wake, inatoa vipaumbele kwa wananchi wake Ila kuna muda sheria zinakua mbele ya kipaumbele hivyo uhai wa raia kusahaulika. Hii ndio sababu leo hii nina andika haya. PF3 imechukua uhai wa nguvu kazi moja.

Mfano wangu unaongelea kwa mtu mmoja, Ila naamini sio huyu pekee aliyepoteza uhai wake kwa sababu ya PF3, bali hata katika jamii zinazotuzunguka wapo watu ambao wamepoteza uhai wao kutokana na kutokua na PF3 pale wanapowahi hospital kunusuru maisha yao.

Naomba niulize tena, PF3 Ni kiungo gani kwenye afya ya binadamu?.

Tanzania tuitakayo itajengwa na watu wenye afya njema. Ikiwa sekta ya afya itachukua hatua mbadala ya kuwapa vipaumbele wagonjwa wanaotakiwa kuwa na PF3 wanapofika hospital wakiwa katika hali mbaya hata bila ya kuwa na PF3 kwa wakati, tutaokoa nguvu kazi nyingi Sana kwa maendeleo ya miaka 5, 10 na 25 na hata zaidi ya 25 Tunayoitazamia.

PF3 tunaomba utuhurumie.

1719767324959.jpg

Chanzo: TBC online media.

Ukiachana na hilo Kuna swala la kulipa pesa ndipo upatiwe matibabu, hili Ni wazo zuri kwani litarahisisha matibabu ya mgonjwa kuwa katika malipo hivyo kuzuia usumbufu pale matibabu yanapokamilika.

Changamoto ipo kwa mtu ambaye amefika hospitali akiwa mahututi ingawa anahitaji matibabu ya haraka lakini mfukoni hana kitu, hii inapelekea huduma kuwa hafifu na dhoofu kwa wagonjwa hao kwani pesa imebeba uhai wao hivyo pasipo pesa inapelekea kuachwa pasipo matibabu na kusababisha kifo, au kupata matibabu yasiyo ya viwango.

Tunaomba serikali itilie mkazo katika hili ili kuokoa maisha ya watu wengi, ikiwezekana kila mtanzania awe na bima ambayo itakua nafuu kuilipia kwa kila mtanzania wa kila Hali. Kwa kufanya hivi tutaipata Tanzania tuitakayo kwa miaka 5, 10 na 25 au Hata zaidi ya 25 Tunayoitazamia.

Afya bora ni haki ya kila mtanzania, kwani kila mtu ana haki ya kuishi. Hivyo basi kwa pamoja tuungane kutokomeza ajali za barabarani kwa kuzingatia sheria za barabarani na kuboresha miundombinu ya usafirishaji, pia elimu kwa madereva itolewe ili kuimarisha usafirishaji Bora na salama.

Kwa kufanya hivyo matumizi ya PF3 yatapungua hivyo kupelekea vifo vinavyotokana na ukosaji wa PF3 kwa wagonjwa wa dharura hasahasa waliofikishwa hospitali kwa msaada wa mashuhuda wa ajali kupungua.

Vilevile kila abiria wa chombo Cha usafiri awe mlinzi wa dereva wake ili kutokomeza uendeshaji wa haraka barabarani, na kutokomeza matumizi mabovu ya barabara kwani ajali hawapati tu wanaosafiri kwa chimbo Bali Hata watembea kwa miguu wanapata ajali hizo kwa kuhongwa na magari yaliyo katika mwendo wa Kasi hivyo kupoteza uelekeo.

Tukiungana kwa pamoja na kuchukua hatua za haraka, kushughulikia tatizo hili hakika ajali barabarani zitapungua.

Naipenda Nchi Yangu.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom