Pf3 vs hospitali

Pf3 vs hospitali

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
7,553
Reaction score
3,081
Habari zenu wandugu. Juzi nilikuwa nasikiliza Clouds wakawa wanaelezea kuna mtoto aliyekuwa analelewa na baba yake mdogo baada ya baba yake mzazi kufariki. Mtoto huyu alifungwa miguu na mikono nababa yake huyu mlezi na kupata kipigo kikali kwa tuhuma za kuiba shilingi 3,500. La kusikitisha zaidi ni kwamba huyu dogo alipopelekwa hospitali akiwa hoi walimkataa kumpokea wakamwambia mama yake kwamba wanatakiwa waende Polisi kwanza kuandikisha maelezo na kupewa hiyo PF3. Wakati wanaenda Polisi mtoto akafariki njiani. wapo wengi wanakufa kwa staili hii

Sasa jamani hii PF3 nani aliiweka na kwanini daktari alazimishwe kuona PF3 Kwanza? Naomba yeyote aliyeweka huu utaratibu uondolewe haraka sana maana wengi wanakufa kwa mtindo huu.Kuna watunga sheria hapa ndani kutoka vyama vyote , tafadhali liangalieni hili swala.
 
Wanafuata sheria namba ngapi, kama ipo irekebishwe. This is against kiapo cha madaktari kuacha mgonjwa afe kwa kisingizio cho chote kile.
 
Kuna sakata la CHOO KIKUU DODOMA ambapo mwanafunzi alicharangwa na wenzie kwa tuhuma ya kuvujisha siri ya mikakakti yao ya kuhakikisha wanamchagua/wanampigia kura mgombea kutoka katika dini yao, akanyimwa tiba kwa siku kadhaa bcos hakupewa pief sree. Ni muhimu wanaharakati walitazame hili.
 
Nakiri kuwa watunga sheria hii walikuwa na nia njema kabisa,lakini kwa bahati mbaya imekuwa kikwazo cha kupata matibabu haraka.Nafikiri kuna umuhimu wa kuifanyia mabadiliko sheria hii kwa kuwa haiendani na wakati!!
 
ngugu zangu wana JF, mwenye kulifahamu jambo hili la PF3 atusaidie kutuelewesha maana ni wengi yanatukuta ,naomba tufahamishwe vyema kama ni lazima uwe kwanza na PF3 ndo mtu apokelewe na kupewa matibabu au anaweza akapokelewa kwanza na wakati anapewa matibabu basi wahusika wafanye utaratibu wa kuishughurikia hayo maelezo toka polisi, na pia atueleze sheria hii ni ya mwaka gani kifungu kipi ktk katiba yetu ya jamhuri.
 
vituo vya polisi viwekwe ndani ya hospitali ili wadhibiti watu wa majeruhi wanaokuja kutibiwa.
Au waajiri madaktari ambao ni maaskari polisi.
 
ngugu zangu wana JF, mwenye kulifahamu jambo hili la PF3 atusaidie kutuelewesha maana ni wengi yanatukuta ,naomba tufahamishwe vyema kama ni lazima uwe kwanza na PF3 ndo mtu apokelewe na kupewa matibabu au anaweza akapokelewa kwanza na wakati anapewa matibabu basi wahusika wafanye utaratibu wa kuishughurikia hayo maelezo toka polisi, na pia atueleze sheria hii ni ya mwaka gani kifungu kipi ktk katiba yetu ya jamhuri.

Hili suala la PF3 ni tata.Sheria inataka PF3 ijazwe na daktari ili kusaidia kukusanya ushahidi ( Forensic evidence) endapo utahitajika mahakamani.Bahati mbaya sana utaratibu huu ukajenga mazoea ya hospitali kudai PF3 na kwa vile PF3 zinapatikana vituo vya polisi tu basi ikawa ni usumbufu au hata kusababisha upotevu wa maisha kama ilivyotokea kwa kesi hii. Kuna uzuri pia wa kudai PF3 kwa maana ya kuwashughulikia wahalifu wanaoumizwa wakiwa kwenye uhalifu.

vituo vya polisi viwekwe ndani ya hospitali ili wadhibiti watu wa majeruhi wanaokuja kutibiwa.
Au waajiri madaktari ambao ni maaskari polisi.

Sasa hivi kuna mazungumzo kuweka hizo PF3 kwenye mahospitali..na huenda likipita hilo basi atakuwepo askari wa kusimamia pia. Ila sijui kama ni practical tukiangalia nyenzo zilizoko.Labda waweke kwenye hospitali maalum.

Kinachotaliwa ni wanaharakati kuendelea kujadili kuonyesha athari zinazotokana na kung'ang'ania PF3 KABLA ya kutoa tiba.Kama sikosei kuna kipindi Waziri wa Afya by then Zakia Meghji aliwahi kusema watu watibiwe ndipo PF3 itafutwe..sina uhakika kama tamko hili lilipewa nguvu ya kisheria au la.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom