Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,081
Habari zenu wandugu. Juzi nilikuwa nasikiliza Clouds wakawa wanaelezea kuna mtoto aliyekuwa analelewa na baba yake mdogo baada ya baba yake mzazi kufariki. Mtoto huyu alifungwa miguu na mikono nababa yake huyu mlezi na kupata kipigo kikali kwa tuhuma za kuiba shilingi 3,500. La kusikitisha zaidi ni kwamba huyu dogo alipopelekwa hospitali akiwa hoi walimkataa kumpokea wakamwambia mama yake kwamba wanatakiwa waende Polisi kwanza kuandikisha maelezo na kupewa hiyo PF3. Wakati wanaenda Polisi mtoto akafariki njiani. wapo wengi wanakufa kwa staili hii
Sasa jamani hii PF3 nani aliiweka na kwanini daktari alazimishwe kuona PF3 Kwanza? Naomba yeyote aliyeweka huu utaratibu uondolewe haraka sana maana wengi wanakufa kwa mtindo huu.Kuna watunga sheria hapa ndani kutoka vyama vyote , tafadhali liangalieni hili swala.