Pfunk na Clouds wapatana

Pfunk na Clouds wapatana

four eyes

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
905
Reaction score
1,408
Kwa wafuatiliaji wa muziki wa bongo flavour jina la pfunky Bila shaka Lina heshima kubwa kutokana na kuwa mmoja kati ya maproducer wa awali wa muziki huo na amewaibua wasanii wengi huku akichangia kuufanya muziki huo kupendwa Kwa kutengeneza beat kali na hatimae nyimbo nzuri,

Kwa upande mwingine redio ya clouds haiwezi kusahaulika pia Kwa nafasi kubwa waliyoitoa Kwa muziki huu na hatimae kuufanya utambe pamoja na kuandaa show nyingi zinazowapa pia rizki wanamuziki wa muziki huu.

Hata hvyo pamoja na mchango wa clouds katika muziki huu bado kumekuwa na lawama nyingi kutoka kwa wasanii,maproducer na wadau mbalimbali kuelekea ktk redio hii kwamba umekuwa na unonyaji wa hali ya juu na kuhusika pia kuwapoteza wasanii wasiokubaliana na unyonyaji huo,mmoja kati ya wadau waliowahi kuitupia shutma clouds wazwaz na kupelekea kuvunjika Kwa uhusiano wake na redio hiyo ni pfunky.

Katika moja ya mahojiano yake alipokuwa akizungumzia kifo cha msanii Albert mangwea,producer pfunky aliishutumu redio hyo kuwa ilichangia kumpa stress mangwea na kupelekea kujiingiza ktk utumiaji wa madawa ya kulevya mpaka kupelekea kifo chake sababu ya unyonyaji wao.

Pfunky alienda mbali zaidi hadi kutangaza marufuku ya nyimbo za kutoka studio yake kupigwa hapo clouds,lakini hivi karibuni pfunky amekuwa akisikika mara Kwa mara ktk redio hyo akizungumzia mambo mbalimbali kuhusu mziki au wanamuziki na kuleta picha ya uhusiano mpya kati yake na redio hiyo,swali ni je urafiki huu mpya wa pfunky na clouds umetokana na redio hiyo kurekebisha Yale ambayo pfunky alikuwa akiyalalamikia au pfunky ameamua kusahau yaliyopita Kwa manufaa binafsi?karibuni wadau tuchambue sababu ya urafiki huu mpya wa clouds na pfunky.
ebbd2f69acc2723255f6af78fbbdc488.jpg
2b02e28b302e16836863bb7ede9e534b.jpg
7d633b2640fbcdebf4567114fedd6245.jpg
801130454c6cefd7c9a744e9a9e6801e.jpg
 
Back
Top Bottom