Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199
Yawezekana akawa na sifa ya kupata PhD ya heshima kama walivopata wengine, lakini nikweli kuna haja ya hizo PhD kuwa nyingi hivi!!!!
Juzi tu ikiwa ametunukiwa PhD ya biashara nchini Uturuki leo hii,naambiwa anajiandaa kutunukiwa PhD nyengine nchini Tanzania, kufanya jumla ya PhD alizotunukiwa kufikia nne (4).
Ni kwa mchango upi na jema lipi kubwa la kustahiki idadi kubwa ya PhD kiasi hiko.Ikiwa yeye ni Rais wa Sita,nyuma yake kuna marais watano waliofanya mambo makubwa mno kwa nchi hii sio tu kiuchumi bali pia kimkakati mapaka kuifikisha nchi hapo ambapo yeye kaikuta,mbona hatukuona wakitunukiwa hizo PhD hata moja moja.
Ni wazi tu kusema ,heshima hii anayopewa SSH ni mbinu tu za kisiasa za kumtafutia namna ya kukubalika na wananchi kisiasa kwa uchaguzi wa 2025.
Na ni wazi kwamba hili linafanyika kwa sababuya kukosekana njia nyengine mbadala ya kutengeza jina ili kumtengezea njia boss wa chama kuweza kukubalika kwenye machoya wananchi,na macho ya kimataifa.
Mm maoni yangu,heshima kama hizi zisitumike kisiasa,kwa kuwa thamani yake yote itapotea na kuonekana ni kitu kisichokuwa na mana na thamani yeyote kwa mtu kuwa nayo katika jamii.