PhD ya Tozo na Kukopa!

PhD ya Tozo na Kukopa!

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Unakaa na kutumia elimu ya PhD kuweka Kodi kwenye matangazo ya akina Juma Lokole! Mtu anapost kutangaza Shanga na Chupi halafu eti naye unamfikiria kama Chanzo cha Mapato!

Tumechoshwa na watu wanaokaa ofisini na kufanya kazi kwa mazowea. Kwanza ilipawa tuelezwe ni kigezo gani kitatumika kumpima mtu kuwa influencer. Halafu utuambie hao influencer wako wangapi na watachangia kiasi gani kwenye pato la nchi.

Bado umepunguza bando la internet, bado vifaa vya mawasiliano unavitwika matozo na huku unataka Kodi kwenye jasho la vijana wanao jitutumua! Watu wamefikia hatua ya kujitoa ufaham na kujiita Chawa nao unaona wivu unataka Kodi toka kwao. Aibu!

Badala ya kuja na Sheria kali ya kulinda mapato yanayopotelea kwenye matumbo yenu, mnakuja kukamua watoto wa maskini!

Hivi mmekosa vyanzo vyenye mashiko? PhD unamuwaza Mwijaku na Babalevo kama chanzo cha mapato? Kwanini usiweke Kodi ya vitambi? Maana navyo mnavitumia kutuibia.

Mnakera sana mpaka kichefuchefu.
 
Pale watu wanaposoma kwa kukariri na sio kwa kupractice... Practical ndio kazini utegemee nini... Maisha mtaani magumu wao kwa kuwa anakaa ktk viyoyozi hawajui jua linavyowaka... Muda utasema... Na mimi nasema iko Siku watu watajuta kuwa hi kuwa viongozi... 😎😎
 
Back
Top Bottom