ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
PHILIBERT KABAGO
"Philibert kabago ni msanii wa kizazi kipya ambae masikani ama chimbuko lake ni kutokea jiji Mwanza, na ni sehemu ya Group members waliounda Crew ya " Boys with Voice" Crew ya "Boys with Voice " ilianzishwa mwaka 1997,Kundi ambalo lilikuwalinapatikana katika kata ya "Kirumba" lakini pia ni miongoni mwa Kata kumi na tisa (19) zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza..
Kwa kifupi Kundi hili liliundwa na Philibert kabago ambae katika hili kundi alisimama kama kiongozi, hamad salehe lakini pia kulikuwa na member wengine katika kundi hili la " Boys with Voice " ambao sauti zao hasikusikika katika nyimbo nyingi za kundi hili la " Boys with Voice"
Kwa mfano msanii kama vile: kazibert muhando ama jina maarufu " K. MO" Na mwingine alikuwa anaitwa " masanja Salum" a.k.a Rasi Masta..
Lakini wasanii ambao wali bahatika kushiriki katika Album ya "Boys with Voice" ( B.W.V) inaitwa " Nawashangaa" . Album hii ilitoka Mwaka 2003 Album iliyokuwa ina nyimbo kama Tisa (9) hivi. ngoma hizo ni kama vile:
1. Barabara zilekebishwe
2. Boss nipe mshahara Wangu
3. Maisha mzunguko
4. Mrembo Wangu
5. Mzee mchana Usiku kijana
6. Leo na kesho
7. wanawashangaa
8. barabara zilekebishwe Rmx
Na nyingine nyingi.
Ni sehemu ya a Album ambayo iliwashirikisha wasanii wengi Tu, nakumbuka katika Album yetu kuna msanii kama " Banana zoro" ambae tulifanya nae katika wimbo unaitwa " Mrembo Wangu" msanii mwingine ni Suma G kutoka Crew ya hot pot family ambae nae sauti ama verse yake ilisikika katika wimbo wetu " mzee mchana Usiku kijana" , kuna Solo Thang ambae tumefanya nae katika wimbo wetu wa " leo na kesho" .. Sarah kipingo ambae tumefanya nae "Barabara zirekebishwe"
Kuna sister p ambae tumefanya nae Barabara zirekebishwe Rmx ...na Crew ya mabaga fresh ambao tumefanya nao wimbo unaitwa " Maisha Mzunguko" kuna marehemu mack 2b a.k.a simba kutoka Crew ya wateule nae pia tulifanya nae wimbo unaitwa " wanawashangaa" hao ni baadhi ya wasanii ambao tuliwashirikisha na ninakumbuka Album hii ilifanyiwa uzinduzi 2003 .
Ilikuwa ni tarehe 13/9/ 2003 katika Eneo moja hivi linaitwa " Country point" Na uzinduzi wa pili ulifanyika Tarehe 14/ 9/2003. katika Uwanja wa mpira unaitwa " Ccm kirumba" na kuna wasanii wa kizazi kipya wakali kibao Enzi hizo walikuja jijini mwanza siku ya Uzinduzi huu ili kutupa Support.. na ilikuwa ni show kubwa sana siku hiyo kuwahi kutokea jijini Mwanza kufanywa namna ile na wasanii hasa wa kizazi kipya.
Event / concert hii ya Uzinduzi wa Album hii ya " Boys with Voice " inaitwa " wanashangaa" ilikuwa na wadhamini kadhaa waliojitolea kufanikisha uzinduzi huu kama vile...
" Radio Free Africa , . Star tv & kiss fm ( Sahara media Group) , maana walitoa ushirikiano kwa kutangaza matangazo hayo live kupitia tv & radio.. na hata promotion wiki moja (1) kabla ya uzinduzi huu kufanyika..
Lakini kwa Upande wa wasanii waliohudhulia Show hii ni kama ifuatavyo.
1. Ay & Buff G
2. Maua
3. Solo thang
4. Jay moe
5. Mr paul
6. Mandojo & domokaya
Pamoja na mwana Dada vick kamata ambae alikuwa bado anasoma katika Chuo cha " Sauti " Enzi hizo nae alitoa support kwetu . Bila kuwasahau wasanii kutoka hapa hapa jijini Mwanza wasanii kama Vile.
1. Jita man
2. Jungle man
3. H. Baba alikuwa ni kama Dancer wetu ,
Baada ya kumaliza kufanya Uzinduzi jijini mwanza, tulifanya tour maeneo kama vile , shinyanga , msoma , kama sehemu ya kuwathamini mashabiki zetu..
Itaendeleaaa..
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202