Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
_
Ilinigharimu muda mrefu sana kumuelewa Stamina shorwebwenzi, aliposema "kama wakati ni fedha basi ningefungua benki ya saa". Nilituliza kichwa nikatafakari, upo uhusiano gani kati ya muda na fedha? Niligundua amehoji kauli ya wazungu 'time is money'. Nilipogundua hilo nikapata maana, ndipo nikapata hiki kichwa cha habari.
Wakati nafikiria kumuandikia Coutinho hiki kichwa cha habari, niliiwaza tena habari ya Gabriel Batistuta. Yule jamaa aliyekipiga Fiorentina miaka ya 90. Fiorentina iliposhuka daraja, yeye aliamua kushuka nao. Akakataa ofa ya kwenda AC Milan, Manchester United na Real Madrid. Akaenda Serie B kupigana na Fiorentina kuipandisha daraja. Kwa ule ushujaa, Fiorentina walimpa heshima ya kumsimamishia sanamu lake mjini Florence.
Ndipo nilipoiwaza tena kauli ya Coutinho ya January 6, 2018, alisema "Naenda Barca kutwaa taji la UEFA". Kauli ngumu sana kwa Liverpool. Yaani aliona haiwezi kuchukua UEFA akiwa na Liverpool? Au alimaanisha nini?
Wakati akiwaza Kuchukua UEFA, Liverpool walichukua pesa waliyolipwa, wakaenda Southampton kumleta Van Djik, alafu Roma kumleta Allison, wakatupa macho kiasi kilichokuwepo kwenye account, wakaenda As Monaco kumchukua Fabinho.
Wakati Liverpool wakifanya hayo, Barca walikuwa bar na glass za champagne, wakijipongeza kumpata Coutinho. Walimuwaza Coutinho wa Etihad dhidi ya Man City kisha yule dhidi ya QPR pale Anfield, wakatabasamu wakijua mbadala wa Iniesta amekuja. Wakamuambia, hongera kwa kuja kutwaa UEFA.
Ila sasa miaka miwili imepita, Liverpool wametwaa ile UEFA aliyoiota, yeye bado anacheza kwa mkopo Bayern. Sasa yupo sokoni, hajui wapi aende akapate Champions League aliyoiota. Anajua ana miaka 27, hahitaji kwenda club wanayojenga timu, hivò ana mtihani mzito.
Kitu pekee kinachoweza kumsaidia Coutinho kwa sasa ni muda, akimtafakari Stamina vizuri, atajua anachotakiwa kufanya.