Philosophers & philologist

Okoth p'Bitek

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2019
Posts
1,124
Reaction score
1,384
Wahuni wa huku wana maneno mengi kuliko vitendo

Wahuni hawajiheshimu

Wahuni wanaomba mungu awalinde
Wahuni wengine wanatutishia kwamba tutaona, vipi kumbe tulikuwa hatuoni au mmelenga kutuonyesha nini?!

Wahuni hawapoi wanapenda mdomo kuliko kula, kila mhuni amewekeza kwenye maigizo yake,

Je ni kweli kuwa ukiingia anga za mhuni hutoki salama,

Mhuni hana sifa moja, amejua kuongea, kwanza anachikipenda zaidi ni kuimba,

Hajiheshimu,
Anatafuta pa kufia,

Kila jipya chini ya jua amepita nalo,

Kwake jukumu sio sifa, yeye cha msingi usimyeyushe.....

Poleni ndugu zanguni, huko mlipo ni maono yangu kuwa mpo salama,
Mungu amenipa kazi ya kuzungumza na ninyi walinzi wake,

Niwapashe juu ya habari, ambayo haitalenga kumuona kipepeo mzuri na mende mbaya lengo ni wote waonekana kwenye mzani unaotoshana,

Malaika walipotua kwenye bahari ya giriki, habari zilifika ulaya yote, na kila mmoja wetu alivutiwa na habari zake, kama ilivyo desturi, watu wa sanaa walijipa mamlaka bila ya ninyi malaika walinzi, na yale maigizo yalichezwa zaidi upande wa roma,

Mtoto akililia wembe mpe, na kweli walimpa akauchezea, ukamkata, na imekuwa shauri lake mwenyewe,

Na hakuna aliyekuwa tayari kuondoa haya makali yaliyopo kwenye wembe, bali kila mmoja amekuwa akifanya kazi ya kuuhamisha,

Na kwa namna unavyokata, sioni kama kuna atakayepona, haya yote mimi hayanihusu, kinachonitatiza, ni hali ya huu ukimya,

Si huwa mnatamba kuwa hamtishiwi na maneno, nyie mtu akiongoea mnamcheki na kumpotezea, imekuwa vipi, leo na nyie mmelaghaiwa na maneno, kwani na kusoma kwenu kote zile njia, ni kwanini mmechagua kuwapitisha watu wangu kwenye njia za nchi ya malaika wa mbali,

Ina maana hamuoni joto au baridi kuwa kikwazo, ni kweli au ndio namna ya kuutafuta ukweli wa kuona matokeo ya kumlisha chui nyasi, ni kwanini asili ilipendekeza utofauti wa rangi, na njama zake zote,

Mziki ulioandikwa na msanii aliyekuwa anaumwa baridi leo umeonekana kuwa mziki wa maana kwa watu wangu wa sahara na mmewahimiza kwenye ngoma wote wafike bila kukosa na ambaye hatafika, atadaiwa na pia anastahili kushitakiwa

Wana mkwara kinoma, mwalimu wao anahisia ya dhambi, na hiyo hisia ameiambukiza kwa watu wote wa kisasa, ndio sembuse, sisi ambao alijua kabisa kuwa anakuja kutuigizia,

Ni nani mwenye jukumu la kufundisha hawa wanyama kuongea mambo yao,
Asili yao,

Kurudi nyuma na kubomoa ulichokijenga ni kama haiwezekani, kwasasa wanazungumza matumaini na imani, na imekuwa ni ngumu kutofautisha mwanamme na mwanamke, matendo yanafanyika mbali, kwa maana kuna mwenye nguvu zaidi yao, je ni mungu au ni just Gap

Wanaojiheshimu, kidogoo ndio wanachanganya,

Watoto wa kwanza wa wale watoto wa Mmiku nyerere leo wamekimbilia india kwa ajili ya kutibu hili tatizo lao la kike, wameanza kunusa, wanaona kinachotokea mbele ya macho yao, wananusa mpaka mwonekano, in short wamekuwa, wanasikiliza japo na mawazo ya awali, kinachowachanganya ni umri wao, wamekuwa watu wazima sasa, wameamua kukubali, yes sayers

Hiki ndio kizazi cha mwisho kukubali kufa na madeni, kwasababu ni kweli kwenye ujana wao walikopa sana, kuhusu watoto wao mimi sijui, ila ni kwamba watazaa waswahili,


Hawa wametumwa na malaika kwaajili ya kutuma taarifa ya kifo cha mungu, wanasema kimebaki kivuli tuu, na kwa kasi ya maigizo sioni kama hiki kivuli kitaendelea kuwepo kwa karne moja,

Wanafanya ubaya wakiwa wanalindwa na mungu, hii imesaidia kuongeza ujasiri wa matendo,

Watoto wao, watajisahau bila kuelewa kuwa wazazi wao walifanyiwa njama ya kupatikana wao, nnasikia wanaonea huruma wanyama, hawali nyama, wanaogopa kuchinja kuku, ni proffesionals, kwao jukumu ni sifa mtu wangu,

Binafsi nimechoshwa na wasomi wenye imani na matumaini, muwafundishe kuona, daktari, mkandarasi, mwalimu, mkulima, wafundisheni kuona tena kwa sauti,

Kwaheri ya kutokuonana
 
Unaongelea nchi au watu halisi mana kwetu sijaona uhalisia hapa labda kwa hii siasa yetu ndo umelenga. Mana umetufunga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…