Phone repair (programs & ma file ya kutengeneza simu)

Phone repair (programs & ma file ya kutengeneza simu)

FOX21

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
493
Reaction score
916
Salamu zangu ziwafikie wote walio jaliwa afya njema na pole kwa ndugu zangu wanao pitia wakati mgumu kiafya hasa wenye homa kali na mafua.
Niende kwenye mada nisiwachoshe Sana ndugu zangu.

Nimeamua rasmi kufanya kazi ya ufundi simu hii ni kutokana na hali ya kiuchumi kuwa tete kwa upande wangu, nimefunguwa ofisi site imechangamka na nimeanza na vitu vichache tu nikiwa na computer pamoja na mashine ya blower.

Asilimia kubwa ufundi simu sijasomea ila najifunza kupitia mitandao ya kijamii, japo nakumbana na changamoto mbalimbali naamini tukiungana ndugu zangu wenye uzoefu ktk nyanja hii nitafika mbali na mm nitafunguwa ajira kwa vijana wenzangu.

Kilichonileta mbele yenu ndugu zangu Nina kumbwa na changamoto ya kupata program au file za kutengeneza cm mfano kuflash, kusetia network, nk.

Kwa yeyote anaeweza kunisaidia au Kama Kuna group linalo husika na maswala haya naomba link either WhatsApp au telegram tuweze kuungana, kushirikiana na kusaidiana Mambo mbalimbali ya kiufundi.

Nashukuru kwa muda wenu🙏🙏🙏🙏.
 
Software tools mkuu.
Ili uweze kufanikiwa kwa urahisi zaidi ainisha aina za simu unazokutana nazo kwenye mazingira yako ya kazi au CPU. Hii itaepusha kuambiwa tafuta tools fulani wakati kwako hakuna aina ya hizo simu ambazo ziko supported na tools.

In addition: aina ya matatizo unayokumbana nayo kwenye simu.
 
namie mkuu..nahitaji kufundishwa kuhsu softwares na kuflash simu zote..Gharama ntalipia[emoji120]
Uko wapi ? Kuna sehemu moja wakati nazunguka maeneo ya mwanza nilikuta wameandikia wanatoa mafunzo ya ufundi simu , ilikuwa maeneo ya ilemela , ni vema kwenda huko ukapata maarifa zaidi , online ni nzuri lakini itatumia gharama kubwa zaidi ila kama una idea ni vzr hata online. Ila upate mtu mwenye specific time yakukufundisha wewe , alikuwepo fundi mmoja sijui alipotelea wapi ?? Kanifunza vema sana sijapata kuonan, yuko bright , ila alivyopotea mtandaoni simpati hata , ningekuunganisha nae , hata uwe na kichwa kigumu kiasi gani utamuelewa .
 
Nenda mliman city Kuna maabara au clinic ya simu sijawahi ona ufundi kama ule tz nii more than professional
 
Back
Top Bottom