Picha: AY na wasanii wengine wakiwa Ikulu ya Marekani

NguoYaSikuKuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
681
Reaction score
1,020
AY ameungana wasanii wengine wakubwa barani Afrika jijini Washington DC, kwa mwaliko kutoka ikulu ya Marekani kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika utakaofanyika wiki hii.

AY akiwa White House

Wasanii hao ni sehemu ya wale walioshiriki kwenye mradi wa One Campaign. Wasanii wengine waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Femi Kuti, Owamumi na D'Banj wa Nigeria, wa Afrika Kusini na Fally Ipupa wa DRC, Victoria Kimani wa Kenya, watakaoungana na mchezaji Manchester City, Yaya Toure mjini Washington D.C. kuanzia August 4-7.

AY akiwa pamoja na Femi Kuti, Victoria Kimani na wengine

Rais Barack Obama atawakaribisha viongozi kutoka barani Afrika kwenye mji huo mkuu wa Marekani katika mkutano wa siku tatu. Huo ni mkutano mkubwa zaidi kuwahi kufanyika kati ya Rais wa Marekani na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali za Afrika.

Kwenye ziara hiyo, wasanii hao watakutana na viongozi wa juu wa serikali Marekani, wajumbe wa taasisi ya Young African Leaders Initiative (YALI) na wajumbe wa Congress. Pia watatumbuiza siku ya August 4 ukiwemo wimbo wao wa ‘Cocoa Na Chocolate'.



ANGEKUWA YULE.........TUSINGELALA MPAKA LEO!!:cool2:
 
Pengine walienda kama watalii, kitu ambacho ni kawaida huko
 
Ngoja na mimi nijipe kazi.

AY ndio msanii wa kwanza Mtanzania kukanyaga white house.

Sisi watoto wa tpanga hatunaga kelele haya ni mambo ya kawaida sana kwetu.

hahahaaaaaa..!!mnaumiza watu roho!
 
Ngoja na mimi nijipe kazi.

AY ndio msanii wa kwanza Mtanzania kukanyaga white house.

Sisi watoto wa upanga hatunaga kelele haya ni mambo ya kawaida sana kwetu.

Akirudi bongo lazima tumpokee na mabango ya ushujaa.
 
Wala sisi Marekan tumeshazoea tangu tuko nursery study tour zetu ni desney land.

wenzenu hawakuwahi kuota wala kuwaza
ni kama coincidence tu ndo maana vtu vdogo vdogo wanashoboka
 
yaaani angetaka mpaka taifa limsindikize airport
mi nasmaga acha kupiga mayowe acheni wayaone!!
wale wapambe wangesema kapiga picha na OBAMA

Nini kupiga picha?kaombwa na namba kabisa
 
Ninavojua mimi hata ndomo alishiriki kwenye ule wimbo,ni kigezo gani kilichofanya aachwe kwenye hiyo listi?au ni.......
 
huyu mshikaji anakubalika sana nje ya mipaka yetu halafu hana kelele..hustle hard until you are no longer have to introduce yourself..
 
Ninavojua mimi hata ndomo alishiriki kwenye ule wimbo,ni kigezo gani kilichofanya aachwe kwenye hiyo listi?au ni.......

wamechukuliwa watu wenye status zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…