Inabidi elimu itolewe juu ya nini maana ya KATIBA,umuhimu wake na mambo mengi yahusuyo katiba.
Watu wengi hawajui nini maana ya katiba na uhusiano uliopo kati ya katiba na maisha yao,isiishie hapo,watu wapewe maana ya TUME HURU YA UCHUNGUZI,na umuhimu wake.
Huwezi kushangaa wananchi hawataki hata kupiga kura,wakijiuliza kwani nikimchagua flani akipita,atanisaidia nini,kwani baadhi ya watu wengi,uelewa wao ni mdogo kuhusu mambo mbalimbali.
Suala la vita dhidi ya ujinga,aliloliasisi Mwl.Nyerere,baadhi ya viongozi wa siasa,hudhani limeisha,wakati kiuhalisia bado limetamalaki.