Picha: Billionea ampangishia Lulu jumba la kifahari

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ' Lulu' , mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha ( jina tunalihifadhi kwa sasa ) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la kifahari .

TWENDENI USHUANI
Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake .

Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze ' vizuri' na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ' kamwendo' . Nje ya nyumba hiyo kuna ' parking ' ya magari madogo zaidi ya kumi huku chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua ya kuvutia. "Amehamia hivi karibuni , anaonekana muda wa kutoka na kuingia tu . "Lulu ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya kupendwa , kwa hiyo siyo mtu wa kukaa uswazi, " alidai mtoa habari wetu na kuongeza : "Bidada kaula maana nasikia jamaa ameahidi kumpa matunzo ya nguvu . "Alianza kwa kumnunulia lile gari la kifahari la Toyota Rav 4 New Model analotembelea Lulu, sasa naona kamuweka pazuri na kweli nyumba inaendana na hadhi yake .

ADAIWA KUMPA JEURI YA KUWAFUNIKA KAJALA , WEMA

"Nasikia jamaa amempa jeuri ya kuwafunika kabisa Kajala ( Masanja) na Wema ( Sepetu ) ambao inasemekana wana mkwanja wa kumwagamwaga ovyo .

LULU LAIVU
Kupitia Kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV , Lulu alionekana ndani ya mjengo huo uliojaa mazagazaga ya thamani. Mjengo huo una makabati makubwa ya nguo na viatu kiasi kwamba mtu unaweza ukahisi umeingia kwenye duka la nguo ( boutique ) na viatu kibao. Akizungumza kwa kujiamini Lulu alisema kuwa anapenda vitu vizuri hasa linapokuja suala la kupiga pamba ndiyo maana amejaza pamba kali kwenye makabati ."Kimsingi sipendi shida, napenda kuvaa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri na mambo yote mazurimazuri , " alisema Lulu. Elizabeth Michael ' Lulu ', akiwa kwenye pozi.

BILIONEA GANI?
Ili kupata undani wa mwanaume huyo, gazeti hili lilichimba ambapo kwa mujibu watu wa karibu na Lulu, jamaa huyo ni mfanyabishara mkubwa wa madini jijini Arusha . "Kama mtakumbuka , huyo jamaa aliwahi kuwagombanisha Lulu na Husna ( Maulid ) kwani mwanzoni alikuwa mwanaume wa Husna. "Hivi unajua kabla ya ishu hiyo.

Lulu na Husna walikuwa mashosti lakini baadaye wakawa kama paka na panya kisa tu ni huyo bilionea , " kilidai chanzo hicho.
LULU ASAKWA
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo ya mtaani, gazeti hili lilimsaka Lulu hadi nyumbani kwake na lilipomkosa lilimtafuta kwa njia ya simu na alipopatikana alifunguka : "Kiukweli kabisa nyumba ninayoishi sasa mimi na familia yangu siyo kwamba nimepangishiwa wala kununuliwa na sijui bilionea au kigogo yeyote , hayo ni maneno ya watu tu . Unajua watu wanaongea sana, wanadhani mimi siwezi kujimudu , " alisema Lulu kwa kujiamini.
 

Attachments

  • 1411716357281.jpg
    63.9 KB · Views: 4,810
TRA waanze kutoza kodi kwa wauza papuchi wote maarufu mjini,wanahongwa majumba,nguo hadi ushuzi na toilet paper halafu wanatutukana sie tunaotumia TECNO na HUAWEI tulizonunua kwa jua na jasho letu!!!

Mkuu fikiria Wema,Kajala,Lulu etc wapewe special TIN # ambapo watalipia 4mln each person kwa 4 installment si zitasaidia kujenga visima sitimbi huko na kuzuia kutupa hela hovyo kwenye vitamasha??!!

Asielipa anazuiwa kusafiri nje ya nchi na akitaka kwenda mkoani lazima akaombe kibali kwa kuwa atakuwa amewekwa kwenye kitengo maalumu cha uchunguzi kufuatilia mienendo ya maisha yake na chanzo cha kipato chake kwani wanatiliwa shaka,hata disco pia marufuku kwani wana bad influence,hawatolipa/kulipiwa tu??!!

Haiwezekani Wema mwenye kaofisi ka computer 2 na kasuzuki kaofisi aseme nyumba yake 400mln! Kanumba kafa bila nyumba na hata Ray hana!!

Haiwezekani Lulu hana hata biashara ya juice ya ukwaju,ubuyu au hata chips kama wapemba na hana hata kazi ya secretary aseme anajimudu kupanga bangaluu,Kanumba kamuua bila hata ya Kibanda!!

Bongo movie kweli kumejaa makahaba,maisha yao maigizo,pesa maigizo,mat@ko maigizo,sura maigizo,waache dharau na hata wakihongwa wafanye vitu vya future!!!
 
Wadada nao sijui wanashindwa kujiongeza au wanafuata masharti, unakubalije kupangishiwa jumba la kifahari badala ya kuopt kujengewa au kununuliwa japo nyumba yenye hadhi ya kati ukawa mmiliki wa moja kwa moja. Unapangishiwa, mkikosana unarudi kijiweni.Siwaelewi wadada wa aina hii.
Hivi siku hiz wanaume ni wagumu kuwanunulia nyumba mademu ni kuwapangishia tu,
Sio Lulu tu pia kuna rafiki yangu kapangishiwa bonge la nyumba
 

Tatizo show off, wanataka waishi kama mastaa wa ulayaa...
 
Mabilioner wa Arusha siyo wale watumiaje wazuri wa v agra! mda wowote wanaweza kukungoa kichwa wale
 

Mi huyo rafiki yangu anaishi na bwanake na wana mtoto mmoja,ngoja tutasikiaaaaa tu ya Lulu
 
Mjini msingi kiunoo...we kalia tu mtaji na faida ufe masikini....

Aku mi msukuma wangu yupoo wa kufa na kuzikanaaaaa wala simpi nya teh teh napewa nachotaka miee
 
Nilishangaa juzi nilivyoona kwenye nirvana,yuko vizuri kwa kweli..nyumba nzuri,hayo mavazi sasa...ila alinikera na kile kiswanglish chake
 
Nilishangaa juzi nilivyoona kwenye nirvana,yuko vizuri kwa kweli..nyumba nzuri,hayo mavazi sasa...ila alinikera na kile kiswanglish chake

Nilicheka kweli hiyo english yakeee
 
TRA waanze kutoza kodi kwa wauza papuchi wote maarufu mjini,wanahongwa majumba,nguo hadi ushuzi na toilet paper halafu wanatutukana sie tunaotumia TECNO na HUAWEI tulizonunua kwa jua na jasho letu!!!

Hahahaha,kweli mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…