Pre GE2025 PICHA BORA: Matukio ya Kuvutia ya kukumbukwa Lissu na Mbowe wakati wa Uchaguzi wa CHADEMA Taifa

Pre GE2025 PICHA BORA: Matukio ya Kuvutia ya kukumbukwa Lissu na Mbowe wakati wa Uchaguzi wa CHADEMA Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chama cha Demokrasia na Maendelea kimefanya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa Chama Taifa, licha ya chaguzi zingine kufanyika ndani ya Chama ila mafahari hawa wawili walitikisa anga la Siasa ndani na nje ya Tanzania kutokana na uswawishi wao mkubwa Kisiasa.

Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Mnyukano wao kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari ilizua hisia kwamba huwenda hata wakikutana uso kwa uso basi wangezichapa ama kutoongea kabisa ila mambo hayakuwa hivyo na kuonesha somo kubwa la demokrasia.

Hapa nimekukusanyia baadhi ya matukio ya picha za kukumbukwa katika uchaguzi huu wa kihistoria katika chama chao;

1. Mbowe, Lissu walivyokutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza kwenye Kikao cha Kamati Kuu Chadema, makuu ya chama hicho, Mikocheni Dar es Salaam, Ijumaa, Januari 10, 2025.


1737720343561.png

2. Tundu Lissu na Freeman Mbowe, wakicheza pamoja kwa bashasha wimbo wa "Tuvushe Mbowe Tuvusheee" kwenye Mkutano Mkuu Bawacha Taifa

1737720359994.png
3. Tundu Lissu na Freeman Mbowe kwenye foleni ya zoezi la kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Mwenyekiti

1737720594282.png

4. Tundu Lissu na Freeman Mbowe wakifurahia pamoja baada ya kupiga Kura

1737720617336.png
Soma, Pia:
 
Kuna mzee mmoja pale ikungi ,ustadhi aliwahi imba shairi Fulani ,anaitwa nani jinalake

dawa za lisu anazijua sana yule
 
Moyo huwa unaongea ukweli kuliko tabasamu la Mdomoni.
Hapo mioyo yao inajuana
 
Back
Top Bottom