Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya 4 Dkt. Gharib Mohamed Bilal katika maafali ya 7 ya kutunuku shahada za Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela amewataka wahitimu hao kuwa chachu ya mabadiliko katika kukuza uchumi wa nchi.