jmushi1
Nimesom michango mingi ya thread hii.inasemwa polisi wameua. Picha pia zipo. Pia kuna taarifa za polisi kupiga mabomu kutawanya wananchi. Kwangu mimi haikuwa black and white kujua ni risasi au bomu ndio limetumika katika mauaji haya. Inawezekana mkuu hasira zilizojaa kichwani mwako kimetafsiri maswali yangu kama dispute lakini kwangu mimi ni kutafuta info. kutokana na mwili ulivyoharibika nimepata tabu kufikia hitimisho kuwa ni risasi, na ndio nikatupa masuali yangu.
Ili kukidhi kiu yako, "nalaani vikali unyama/uharamia/mauaji haya yaliyofanywa na wale ambao tunategemea watulinde.
Lakini tusiishie kwenye kulaani tu.Tuhakikishe haki inatendeka. Mwandishi hakuwa na silaha kwa hiyo hakuwa tishio kwa kundi/kigenge cha askari polisi waliomzunguka. Ushahidi unaonesha ni intended murder!