PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Nafikiri hiyo ilikuwa bahati mbaya, kwasababu ninavyoone imetokea, hiyo bunduki kwanza si ya risasi, ni ya mabomu ya machozi kwa wale wanaofahamu bunduki watakubaliana na mimi...

Hilo bomu la machozi wakati mwingine huwa linalipuka vibaya, na nionavyo mwili wa marehemu hapo umesambaratishwa kama na utumbo unaonekana na kuna askari mmoja kwenye hizo picha amedondoka chini kama askari wenzie wanamsaidia vile...

Hebu angalia vizuri..inaonyesha ni kama hapo ilo bomu limefyatuka kwa bahati mbaya likajeruhi marehemu na askari....ni maoni tu lakini....na hawa polisi wetu ambao wametoka depo juzi tu hawa hawajui hata madhara ya hizi vitu.
 
Halafu wakatae waseme ni bomu lilirushwa na Chadema, unyama huu utawatokea kwenye tundu zote za miili yao, kuanzia na amiri jeshi mkuu na IGP
 
Ni usiku wa huzuni sana! What goes around comes around.
 
Kazi ipo...polisi wameanza kujisahau wanatakiwa kufanya nini. Wanatengeneza tatizo kubwa litakaloweza kabisa kupoteza credibility ya jeshi hilo mbele ya watanzania.Mwenye macho haambiwi ona
 
Kamanda weka wakikufungia utabadili jina mbona mimi aipiti wiki mbili lazima wanifungie manake siwezagi kuvumilia ungese ngese wa watu wengne humu ndani kama ritz,mbopo,pasco utakuta na hili wanatetea polisi hakuna mabwege kama hawa..
 
Huyo jamaa aliyemwelekezea bunduki ndio aliyefyatua nini.!! Duh!!, hawa jamaa sidhani kama ni watanzania.
Halafu mwangalie huyo mwenye form vi ya light blue ya mikono mierefu mwenye mapete...mkono wa kulia ameshika bastola kabisa...Safari hii Mungu amewaweka uchi.
 
huyo aliyewekewa bunduki tumboni ndo marehemu? tumekwisha!hii haifai,jeshi la polisi halifai!huu unyama huu ndo mwanzo wa kuiondoa serikali.Hakuna uhalali wa kutawalia kwa namna hii!

Marehemu alikuwa kashikilia kamera yake. Picha wamepigwa huku wakiona kuwa waandishi tulikuwa tukichukua tukio zima, hawakujali.
 
Duh!!Nao walikuwa wanaua huku wanapigwa picha?Huku ni kujiamini over kujiamini!!!
Hii kwa kweli ni mbaya sana!!!!!!

Sasa nimeshaamini adui namba mooja wangu Tanzania ni CCM na Police..Popote nikimwona Polisi ni sawa na nimemwona Nyoka mwenye sumu kali..unajua kinachotakiwa kitendeke kwa nyoka mwenye sumu kali?
 
Ieleweke wazi kuwa mkakati wa CCM ni kuwaua viongozi waandamimizi wa CDM ambao ni Mbowe,Slaa,Lema, Mnyika na Tundu Lisu ambao wamekuwa ni tishio kwa ustawi wa CCM!
 
Asante sana mkuu....huu ni ushahidi tosha...haiwezekani mtu mmoja ashambuliwe na Askari wengi namnahiyo wakiwa na silaa nzito hivyo as if kama ameiba 2billion.

Nashindwa kushawishika kuwa Mwangosi ameuwa kwa kuhudhuria ufunguzi wa tawi la Cdm kuna issue nyingine kati yake na polisi.So sad!
 
Askari alimlima bomu la machozi marehemu tumboni kwa kudhamiria,chini,nyuma ya askari aliyekuwa akijaribu kuzuia kipigo kisiendelee kwa marehemu.Hakukuwa na sababu ya kumwua kwasababu tayari alikuwa under police custody,walitumwa kuuwa!
 
Hiyo picha yako itakuwa ni diffence ya polisi, marehemu anaonekana kakamata silaha ya askari.
Hapana, alichoshika mkononi ni kamera yake ya kuchukulia video na si silaha.
 
Ubungoubungo

acha pumba,silaha ya bomu la machozi inaelekezwa tumboni?huoni ameielekeza tumboni at a close range?acha ujinga ni heri ukae kimya!
 
Last edited by a moderator:
Propaganda za kijinga hizo, ni wapi hizo picha zinapoonesha wameuwa?

Muuwe nyinyi halafu mje kudanganya humu? tutawakamata tu.
Mko tayari kuangalia picha ya maiti ikiwa imesambaratika utumbo? Kitaaluma haturuhusiwi kufanya hivyo.

Mkuu, mimi si mwanasiasa, ni mwanahabari hivyo propaganda si sehemu ya kazi yangu. Siku ukiuliwa wewe pia nitawasilisha habari bila kuangalia itikadi zako
 
Inauma sana jamani..!!?
Ina maana wamemwua huyu mwandishi akitekeleza majukumu yake.??
R. I. P mwangosi.
 
Ubungoubungo

Unasema bahati mbaya, kulikuwa na haja gani ya polisi zaidi ya sita kumkamata mwandushi wa habari?? Acha kufikiria kipuuzi wewe!! Eti bahati mbaya!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…