PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa


Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie - Daudi Mwangosi Apumzike kwa Amani . Amina.
Sii rahisi wenyeji wakamfahamu maana chama Cha siasa kinapotangaza fujo na maandamano Askari wengi hupelekwa kwenye eneo husika toka mikoa ya Jirani.
 
rest in peace Mwangosi, na Josephat Isango kidogo wamuue ila waliogopa kuwa wako DAR
 
Na Jana wametaka kumtoa macho mdada wa watu wa gazeti la Hoja, ambalo wao ndio wanalolimiki...lakini hawaridhiki tu....Ndo maana wameanza kutengenezewa mabomu...
 
Hatutalisahau kamwe tukio hili. RIP mwangosi. Washenzi walikatisha maisha yako bira huruma! Ila nao ipo siku watakufa na wanalo la kujibu duniani na mbinguni!
 
Inasikitisha sana haya mauaji yanayofanywa na Polisi huu ni ugeukwaji mkubwa sana wa haki ya binadamu.
Polisi wajue wanachotukifanya sio kutisha wala wala kuwafanya watu wasidai haki zao za msingi mbali ni kusabisha chuki na mwisho wa siku vita na hali ya kutokuwa na utulivu kama tunavyona kwenye nchi za wenzetu.
Huwezi ukanyima uhuru na kuminya demokrasia ya watu na ww ukawasalama.
CCM mjifunze kwa nchi ziliotumia ubabe na kuminya demokrasia ya wananchi mwisho wao ni kutokuwa na utulivu na vita.
wasikiliseni wananchi mkitaka amani ya nchi hii idumu.
Tulinde amani ya nchi yetu kwa kukuza demokrasia na kuheshimu haki za binadamu.
 
Daaah nchi ya kitu kidogo hakuna kesi wameua wanaishi na kuendelea kuchukua salary kodi zetu zinaendelea kuwalipa
 
Hatutalisahau kamwe tukio hili. RIP mwangosi. Washenzi walikatisha maisha yako bira huruma! Ila nao ipo siku watakufa na wanalo la kujibu duniani na mbinguni!
 
Umenikumbusha mbali. Nimesikitika Sana. Hili tukio nadhani ndo inamfanya mh. E. Nchimbi ashindwe kuingia UKAWA, maana alikuwa waziri wa mambo ya ndani kipindi kile.
 



Hii inasikitisha sana na nakubaliana na wewe kwamba wanahabari inabidi tuendelee kupiga kelele mpaka kieleweke. Pamoja na hilo, ningependa kufahamu ni nini Channel Ten imefanya katika kuhakikisha kwamba haki hatimaye inatendeka? Maana, Mwangosi alikuwa ni muajiriwa wao, na ameuwawa akiwa kazini. Nijuavyo mimi kwa mfano, wanahabari wa Aljazeera waliwekwa kizuizini kule Egypt kwa sababu za kisiasa, na Aljazeera waliendelea kufuatilia kesi yao, na kizuri zaidi waliendelea kuhesabu siku na kutangaza habari hiyo kila siku mpaka kikaeleweka. Sasa kama Channel Ten wameshindwa kufuatilia haki ya mpiganaji Mwangoi, je wanashindwa haka kupiga kelele kwenye chombo chao cha habari kila siku? Hii itasaidia sana kuhakikisha haki inatendeka.

Asanteni
 
R I P mwangosi,, inaonyesha hawa police walidhamilia kumuua na mpaka sasa hakuna aliye ajibishwa huhusiana na tukio hili... Serikali ya ccm imefanya dhambi nyingi sn Mungu kashailaani, lazima itoke madarakani ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…