KWELI Picha hii iliyopigwa kwenye michuano ya Olympics nchini Ufaransa

KWELI Picha hii iliyopigwa kwenye michuano ya Olympics nchini Ufaransa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekutana na picha hii mtandaoni inayodaiwa kupigwa Julai 30, 2024 kwenye michuano ya Olympics inayoendelea. Binafsi siamini, naona kama imetengenezwa.

JamiiCheck tusaidieni kuihakiki.

66a8cb52c4c33.image.jpg


 
Tunachokijua
Kuanzia Julai 30, 2024 kumeibuka picha ya mtu ni anayeonakena kuwa mchezaji wa Mawimbi (Surfing) akiwa amesimama hewani juu ya bahari huku kifaa chake pia kikionekana kimesimama hewani.

Katika kufuatilia uhalisia wa taarifa hii JamiiCheck.com iliipeleka picha hii kwa wadau wake wa mitandao mbalimbali.

Uchambuzi wa Wadau wengi wa umeeleza kuwa picha hii ni halisi na imepatikana kwenye mashindano ya Olympics ya mwaka huu 2024 inayoendelea nchini Ufaransa.

Aidha, Mdau wetu wa Instagram anayetumia jina la Its_E.z.e kupitia chanzo cha The Guardian anaeleza kuwa picha hiyo ni ya mwanamichezo Gabriel Medina raia wa Brazil ilipigwa Tahiti kwenye mashindano ya Olympics ya mwaka 2024 mpiga picha mashuhuri wa aitwaye Jerome Brouillet.

Ufafanuzi wa Mdau huyu wa JamiiCheck hautofautiani na taarifa iliyotolewa na Jariba la The Guardian na Tovuti ya AFP, ambazo zote zinakubali kuwa picha hiyo ni halisi na ilikuwa ni tukio lililofanywa na mwanamichezo Gabriel Medina katika michuano ya Olympiki inayoendelea Ufaransa mwaka huu 2024 na ilipigwa na Mpigapicha mashuhuri Jerome Brouillet

1722442960531-png.3057877

Gabriel Medina

1722443262591-png.3057880

Jerome Brouillet
kushoto, Picha ya Gabriel Medina upande wa kulia
Kwa upande wake mpiga picha Jerome Brouillet kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram (huu hapa) amethibitisha kuipiga picha hii kwa kuweka andiko la kumshukuru Mungu kumuwezesha kupiga picha hiyo ya kipekee. Akielezea kuhusu picha hii katika andiko lake Jerome Brouillet anasimulia:

Nimeguswa na neema. Napenda kusema kwamba kupiga picha ni kama kuvinjari. Ni mchanganyiko wa maandalizi, kujitolea, muda mwafaka, uzoefu kiasi na bahati kidogo.
Mnamo Julai 29, 2024, saa 12:23 asubuhi, tulipofika kwa boti, tulijua ingekuwa siku kubwa ya michezo ya Olimpiki ya kuvinjari. Saa 3:30:31 asubuhi, Gabriel Medina alichukua wimbi bora la siku kwa safari kamili.Saa 3:30:38 asubuhi, aliruka kutoka kwenye wimbi na kusherehekea, sherehe ambayo ilisambaa kote duniani mara moja.Dakika 10 baadaye, simu yangu ya mkononi ilianza kuashiria ujumbe. Bado haijasimama.
Siku hiyo, Gabriel alikuwa majini mahali sahihi, wakati sahihi, na nami pia nilikuwa hapo. Hongera Gabriel.

Pia, ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hii ni halisi na ilipigwa kutokana na video iliyopo kwenye video iliyoambatanishwa kwenye uzi huu hapo juu.
Nilikuwaga nawasikia wazazi wakisema hawa wazungu wameshiba
Mpaka leo sijajua walimaanisha nini
 
Halafu huyu jamaa kabla ya kuja Olympics, walimzuia kutumia surf board yake ambayo huwa ina mchoro wa Christ The Redeemer
 
Back
Top Bottom