Picha Hii Inastahili Kutundikwa CCM Makao Makuu Dodoma

Picha Hii Inastahili Kutundikwa CCM Makao Makuu Dodoma

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA HII ILISTAHILI SANA KUWAPO CCM MAKAO MAKUU DODOMA

Picha hiyo hapo chini ina historia nzuri ya Dodoma kwanza kwa kupatikana kwake.

Nilipokuja Dodoma kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1980 kuja kufanya utafiti Maktaba ya CCM nilikutana na mtoto wa Iddi Faiz Mafungo jina lake Faiz.

Faiz alikuwa ameajiriwa na Shirika la Posta hapa Dodoma.

Alipojua kuwa nimekuja kufanya utafiti wa historia ya TANU akanipa picha hiyo hapo chini lakini nakala yake ilikuwa imechoka sana.

Naiweka hapa ili msomaji apate kuiona.

Faizi akanieleza kwa urefu historia ya baba yake kuanzia alipokuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) hadi hadi kuwa Mweka Hazina wa TANU na jinsi na alivyopewa jukumu la kuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1956.

Hiki ni kisa cha kusisimua na nimekieleza mara nyingi sana.

Hiyo picha ya kwanza ambayo ndiyo nakala nzuri hii picha alinipa Araf Sykes mtoto wa Ally Sykes miaka mingi baadae.

Baada ya kifo cha baba yake mwaka wa 2013 Araf aliingia katika Maktaba ya Picha alizokuwa amehifadhi baba yake na ndipo alipoikuta picha hii akaniletea.

Picha hii ilipigwa Dodoma Railway Station inakisiwa mwaka wa 1955.

Kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu.

Hawa walioko katika picha hii ikiwa mtafiti atanyanyua kalamu kuandika maisha yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika basi ataandika kitabu kizima au sura nzima katika kiitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika.

Picha hii si picha kutokuwapo imetundikwa CCM Makao Makuu Dodoma.

(Picha hizi ni kwa hisani ya watoto wa wapigania uhuru Faiz Iddi Mafungo na Araf Ally Sykes).

1738901098120.png

1738901202789.png



 
Back
Top Bottom