Picha hii inatoa ujumbe Gani kwenu?

acheni kufanya mambo kwa hisia ....unajenga hoja kwa kuhisi , utapata ufumbizi wa kuhisi.
 
JK anajaribu kudadisi kwa nini Karume hayupo kwenye Jezi za chama kama wenzake wakati yeye ndo Kiongozi wa Juu kabisa wa Chama na Serikali kule Zanzibar???...Karume anamjibu, ati mbona Ben ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa hajavaa Jezi kama Mzee Ruksa???

Ben hajapendezwa na hilo jibu...kaonyesha hamaki...na kuguna,...Yusufu kama kawaida yake anaropoka "ebu jifunze majibu mathuri kwa nkubwa wewe!"...Pius anajisikia vibaya na kuangalia pembeni akiwaza "kumbe ndo mana huwa hutaki kuuzulia vikao vya chama???""..na sijui muafaka ule wa CCM na CUF kule kwenu unaoung'an'gania matokeo yake ni nini kwenye muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano!"..
 
Ina maana hivyo viti viwili vilikosa watu au vp? Karume kama anabeba makabrasha ili aondoke???
 
Mh wanafki watupu hao🙁

Ni dhahili kutokana na hii picha kuwa hawa jamaa hawaaminiani ila wanavumiliana tu na hasa wazenj ndio wanaonesha wazi wazi kuwa hawako pamoja na wabara na tofauti hiyo wanaionesha kwa kutovaa kijani!!
 
Picha ninayopata mimi ni hii: This is the Inner Sanctuary...women are not allowed. Not even to serve tea or distribute papers
 
Ina maana hivyo viti viwili vilikosa watu au vp? Karume kama anabeba makabrasha ili aondoke???

Kimoja cha Komredi Shamhuna na cha pili cha Dk gharib bilal (ambaye hawaivi na Dk Karume).
 
Wanajadili jinsi ya kuchukua chao mapema.Wanagawana keki yetu ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…