Picha ninayoipata ni kwamba tangu nikiwa mtoto mdogo, nimeona picha ya baadhi ya wajumbe kama akina Msekwa, mwinyi Mkapa na wengine wengi, badala ya kutumia taaluma na wataalam wa ndani, kuandaa mambo kwa kutumia utaalam, wanapiga porojo na kujisifia tu wala hamna kinacho zungumzwa. Usishangae wanakuja na hoja ya kilimo kwanza bila kufanya upembuzi yakinifu. Kweli kilimo cha kutegemea mvua! ( hapa mvua isipo nyesha hamna kitu), pia barabara zetu za vijijini!(ikitokea mvua ikanyesha, utashangaa magari hayawezi kupenyeza ili mazao yapelekwe sokoni na hivyo wakulima wanayasomba kwa vichwa vya binadamu. hili lipo mpaka leo). Utaalam wa kilimo duni!(wakulima wanakwenda mashambani kwa mazoea. Mtu amezaliwa kijijijni alipo kua akakuta kila asubuhi anakwenda na jembe la mkono shambani bila hata kunywa chai, nguvu hana "Its a lot of frustrations! you can't finish to explain". Ndo maana mmoja amekaa kama kabanwa mkojo!