POTOSHI Picha hii inayodaiwa ni watu walienda kwenye interview ya TRA

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Je picha hii ni halisi au sio halisi? Hawa watu ukiwaangalia vizuri sura zao kama zinafanana hasa wanaume, hata nguo walizovaa wengi zinafanana, na kikawaida mistari haiwezi kunyooka kiasi hiki.



​
 
Tunachokijua
Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku pindi tu, inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Tarehe 06 hadi 19 Februari, 2025 Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Tanzania ilitangaza nafasi za kazi 1,596 katika fani mbalimbali ambapo maombi ya kazi 135,027 yalipokelewa na kupata waomba kazi 112,952 waliokidhi vigezo vilivyowekwa na hivyo kustahili kuitwa kwenye usaili.

Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni ikionesha watu wengi walio katika mistari mireefu ikidaiwa ni foleni ya walioitwa kufanya usaili ajira za TRA kituo cha Chang'ombe


Uhalisia wa picha hiyo.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa picha hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba.

Aidha picha hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambapo baadhi ya watu waliopo katika picha hiyo wanaonekana kuwa na kasoro katika sehemu za viungo vyao vya mwili. Macho kutokuonekana kwa baadhi ya watu, maumbile ya vichwa yasiyo halisi, uwepo wa watu walioungana, yanadhihirisha kuwa ni picha ya kutengenezwa.

Aidha kifaa cha utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba kinabainisha kuwa asilimia 99 picha imetengenezwa kwa teknolojia hiyo.
Je picha hii ni halisi au sio halisi? Hawa watu ukiwaangalia vizuri sura zao kama zinafanana hasa wanaume, hata nguo walizovaa wengi zinafanana, na kikawaida mistari haiwezi kunyooka kiasi hiki
 

Attachments

  • Screenshot_20250331-205502_1.jpg
    393.6 KB · Views: 51
Watanzania hawana nidhamu ya kupanga mistari iliyonyooka hivyo na kusubiriana. Kuna nchi wanapanga foleni hadi kwenye usafiri wa umma....Bongo ikija daladala watu wanaingilia dirishani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…