KWELI Picha hii si ya Tanzania ni kutoka nchini Nepal

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu nimekutana na hii picha yenye mandhari ya kuvutia sana. Navutiwa sana kuishi maeneo yenye utulivu na mvuto kama huu. WanaJamiiCheck naomba mnisaidie kujua hapa ni wapi?

​
 
Tunachokijua
Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.

JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.


Mfano tutumie picha hii inayoonesha mandhari ya milima mirefu pamoja na makazi ya watu yaliyo karibu na mlima hiyo. Je, ilipigwa wapi na lini? ina uhusiano wowote na Tanzania?

Uhalisia wa picha

Jamiicheck imejiridhisha kuwa picha hiyo ni halisi. Kwa kutumia Google Reverse Image Search imebaini picha iliyopigwa Juni 23, 2013 na kuchapishwa katika tovuti ya Flickr mwezi Julai 06, 2013 na Sharada Prasad CS ambaye anabainisha kuwa eneo hilo ni Thånkot, Madhyamanchal, Nepal.

Hivyo picha hiyo hiyo si kutoka Tanzania.​
kwa kutumia nyenzo ya google image search na yandex inaonesha kuwa picha hii haijapigwa nchini tanzania bali inapatikana nchini nepal ambalo linahusishwa na kilimo cha mpungana kuhifadhi chemichemi.
kando na hivyo bonde hili linapatikana katika milima ya himalaya ukanda wa ardhi ambao unaJulikana kama midhills
Licha ya hivyo picha hii imepakiwa katika mtandao wa flicker na Sharada Prasad CS / Flickr .
 
Rungwe Mbeya hapo km sikosei kuna hilo bonde la chai
 
Kinacho sikitisha tunaharibu sana mazingira hasa vyanzo vya maji, hii husababisha mandhari nzuri kama hizo kupotea nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…