SI KWELI Picha hii ya watu waliotumika katika ujenzi wa Pyramids Misri 2549 BC

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
​
 
Tunachokijua
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X amechapisha taarifa iliyoambatana na picha ikielezea ni ya tukio la wakati wa ujenzi wa Mapiramidi nchini Misri iliyopigwa mwaka 2549 kabla ya kristo (BC).

Uhalisia wa picha hiyo

Picha inayowaonesha watu wakiwa wameinua mawe na kudaiwa kuwa ni Wamisri waliokuwa wakijenga mapiramidi ya nchini humo mwaka 2549 kabla ya kristo, si ya halisi.

Picha hiyo imekuwepo mtandaoni takribani kuanzia mwaka 2023 ambapo watu wengi waliisambaza na kuweka madai hayo kama yaliyosambaa tena 2026.

Picha hiyo licha ya kuwa imekuwepo mtandaoni kwa muda mrefu lakini si halisi bali ilitengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya Akili Unde.

Picha hiyo ina baadhi ya dosari mathalani baadhi ya watu hawana viungo vya mwili ikiwemo mikono na vichwa, matendo wanayoyafanya pia yanakosa uhalisia.


Nyenzo za kidigitali ikiwemo Hive Moderation imebainisha uwezekano wa takribani 99% kuna uwezekano wa picha hiyo kutengenezwa na AI.

Aidha kumbukumbu zinaonesha kuwa hakukuwa na kamera kipinda cha Kabla ye kristo (B.C), na picha ya kwanza iliyofanikiwa kupigwa ilikuwa ni ya mwaka 1826 ama 1827 na Joseph Nicéphore Niépce
Hata ukiwa mpumbavu huwezi kuamini huu upuuzi, labla uwe ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…