PICHA: Huyu hapa ndio Binti wa kwanza wa Ndugai. Aumizwa sana na wanaomsema vibaya Mitandaoni baba yake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Huyu ndiye Binti wa Kwanza wa Mheshimiwa Jobu Ndugai ambaye amefariki Dunia hapo Siku ya Jana.

Embu soma kama ilivyo. Mimi nimeichukua kama picha ila ni Video ya Dakika saba binti Wa Marehemu Ndugai akielezea kwa hisia kali sana na uchungu sana juu ya kifo cha Baba yake na Maneno ya Mitandaoni.👉Catherine Ndugai,Mtoto wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Dodoma amezungumza na kueleza jinsi alivyokutana na Baba yake kwa mara ya mwisho kabla ya kifo chake.

Akizungumza na Ayo TV leo akiwa Mkoani Arusha amesema kuwa yeye hakuwahi kutamani kuingia kwenye siasa na wakati mwingine huwa akiona maneno yanayotolewa kwa wanasiasa hata kama hayamhusu baba yake huwa yanamuumiza.

Aidha, ameeleza kukerwa na baadhi ya watu wanaomzungumzia vibaya Baba yake kwenye Mtandao na kusema hizo ni hisia binafsi za watu na haziwezi kumuathiri kwa kuwa alikuwa anamfahamu Baba yake vizuri
#MillardAyoUPDATES

 
Pole kwake,ila mimi pia Nakulaumu hata wewe Lucas Mushambwa kwa kushindwa kujua hali kama hizi za kulifedhehesha familia za viongozi na familia zao zingeweza kutokea kwa ushabiki hata kwa yale ambayo yakionekana kuwa makosa dhahiri,kwa waliona mamlaka,na kama watumishi wa Watanzania na umma.Huku ikisahaulika kuwa kiongozi ni kioo,pale taswira inapoonekana ni mkaa au weusi unatarajia mwitikio gani kwa jamii iliyoamini kioo kimechafuka?
 
Na aumie zaidi. Hata baba yake aliumiza watu na familia zao.
 
Bado samia wako
 
Asijali, kifo ni kifo tu. Kama anaweza aiombe serikali tukufu ya CCM izime mtandao kipindi hiki cha msiba mzito kwa taifa itakuwa kheri.
Ila kama hisia binafsi za watu wa mtandaoni haziwezi kumuathiri sasa kwanini anaumia??!! Sote tutakufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…