PICHA: Ijue BMW 7 Series (Maelezo Mafupi)

PICHA: Ijue BMW 7 Series (Maelezo Mafupi)

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
IJUE BMW 7 SERIES- Kwa ufupi

Na KIMOMWE MOTORS (T) LTD- Waagizaji Magari

UTANGULIZI

Ni moja ya gari za starehe iliyoboreshwa kwenye mambo mengu na iliingia sokoni kwa mara ya kwanza 1977. Leo tutaongelea generation ya 4 iliyoingia sokoni kuanzia 2001 mpaka 2008 inayoshindanishwa na Benz S Class, Audi A8, na Majesta kwa mbali kwa upande wa Toyota.

Injini+Mafuta
Injini zake ni V6, V8 au V12 zenye code zinaanzia 730 mpaka 760 nyuma ya bodi. Injini ndogo kabisa ya V6 yenye umeme mwingi ndio inayotumia mafuta kidogo zaidi kiasi cha km 7-11 kwa lita kutegemea na barabara.

Utulivu na Uimara
Uzito wake wa tani 2 na kuikarikia lami kunaifanya itulie kwenye mwendo mkali wa mpaka speed 260 wakati katika vumbi sio nzuri sana kwa kua iko chini.

Vifaa
Vifaa vyake sio vingi ingawa baadhi vinaingilia na BMW 5 Series haswa injini ya Cc 3000 (306s) inayopatikana pia kwenye X3. Bei ya vifaa vyake kwa ujumla ni juu japo vinadum kwa mda mrefu.

Nyongeza
Push 2 Start, Sunroof, Full Options, Handbreak Button, Options za viti kwenye milango, Camera mbele na nyuma, viti vya ngozi, Long Wheel base, Gia ya kuzunguza kama feni😊, kupokea sim, Screen kwa abiria wa nyuma, Airbags 8 zinazokinga mpaka miguu na mabega na nakshi ya mbao.

Maoni na Ushauri
Anayehitaji gari hii vizuri apate injini code 306s inayopatika kwenye X3 na X5 yenye Cc 3000 sababu ni rahisi kutengenezeka na matumizi ya mafuta sio makubwa sana na vifaa vyake ni vingi kwa TZ.

Gharama
Kuagiza kunagharim kuanzia 33m kwa Right Hand, wakati Left Hand inaanzia 27m
 
Sifa kubwa ya Magari ya mzungu ni uzito na hii inasaidia Sana Kwenye stability.

gari kama Volkswagen golf GTi ina uzito wa kg 1490 yaani inafanana na Subaru forester 2008-2014,wamilliki wa Magari ya mzungu wanainjoi Sana barabaran
 
Wakuu mnahama mada.ila comment zingine ni hatari na nusu.
 
Back
Top Bottom