Picha: kitchen Party ya Lucy Komba ni shidaa

Picha: kitchen Party ya Lucy Komba ni shidaa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.

Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida , wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria.

Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa ( Lucy ) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu ( guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni.

Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.

Akiwa kwenye usafiri wa baiskeri ya matairi matatu maarufu kama ' Guta ' . Kama hiyo haitoshi , Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.

"Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni , " alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.

Ulipofika wakati wa kufungua shampeni , nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.

Akiingia ukumbini kwa mbwembwe. Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi.

Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley , raia wa Denmark . Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark .
 

Attachments

  • 1409728043757.jpg
    1409728043757.jpg
    96.6 KB · Views: 4,016
Mimi nikisika mtu anataka/kaolewa na mzungu sina imani na 0713 yake kabisa........
 
Nashangaa anataka kuolewa na mzungu,wakati last time alikua anatoka na msanii mshamba anaitwa TOX STAR..
 
Hamna kitu subiri tusubiri ya diamond na wema(boss lady) jiji lazima litingishike.
 
Mwenzake Uwoya alipanda kwenye Ngamia ila leo yupo yupo tuu sasa na wewe leta mbwembwe halafu harusi ifanyike then bado tukuone Leaders kila weekend.
 
Mbona picha ni moja tu, binamu tuwekee picha zingine basi warumi
Cc:Tyta
 
Last edited by a moderator:
Huyu atleast anaweza kudumu na ndoa, japokuwa nilisikia pia alikuwa anachepuka na mume wa uwoya ndikamana.

Halafu huyu si alizaa na mdogo wake mume wa Flora Mbasha?
 
Mimi nikisika mtu anataka/kaolewa na mzungu sina imani na 0713 yake kabisa........

Hata miee...pia huwa nahisi midomo yao itakuwa na sugu za kulamba ice cream za baridi....
 
Mbona picha ni moja tu, binamu tuwekee picha zingine basi warumi
Cc: Tyta

Bora umuite Tyta halaf hii ndo kazi yake ujue nashangaa yuko shallow kwel, nilijaribu ku download sasa nikitak ku upload humu sizion ebu ngoja
 
Last edited by a moderator:
Dah yaani maneno yoooote hayo alafu picha moja tu????????????!!!!!!!

Ahahaha hahahah ahaha no zipo wamepiga kama nne ivi na zinavutia kwa kwel, sema nimejaribu ku download nashangaa napat access ya ku upload picha moja tu, halaf hili tatizo la muda sijui kwa nini,yan siwez ku upload picha zaidi ya moja kweny thread
 
Mwenzake Uwoya alipanda kwenye Ngamia ila leo yupo yupo tuu sasa na wewe leta mbwembwe halafu harusi ifanyike then bado tukuone Leaders kila weekend.

Ahahaaa ahaha na sisi tunampa kitchen party apa ahaahah
 
Back
Top Bottom