PICHA: Maisha ya Stephen Keshi enzi za uhai wake

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253


Keshi, nahodha wa zamani wa kikosi cha Nigeria, alikuwa mmoja wa watu wawili pekee kushinda michuano ya kombe la bara Afrika akiwa mchezaji na kocha.



Alikuwa mkufunzi wa kikosi cha Nigeria kwa vipindi vitatu ,na kuisaidia Nigeria kufuzu katika michuano ya bara Afrika 2013 nchini Afrika Kusini pamoja na kombe la dunia mwaka 2014 huko Brazil.



Pia alifunza Togo na Mali,na aliwahi kuichezea timu ya Anderlecht ya Ubelgiji.


Keshi (kulia) na Daniel Amokachi.

Akiwa mchezaji ,keshi alikuwa katika kikosi cha Super Eagles kilichoshinda kombe la bara Afrika mnamo mwaka 1994 na kushindwa kushirki katika mechi za robo fainali za kombe la dunia mwaka huohuo.



Keshi anadaiwa kuugua mshtuko wa moyo, kulingana na vyombo vya habari vya Nigeria.



========

Kifo cha huyu jamaa kimenigusa sana, ingekuwa uwezo wangu ningepanda hata pipa nihudhurie mazishi yake na kuwapa pole wanaijeria.
 
Mwenye picha akiwa mchezaji atupie hapa, tujikumbushe
 
Apate pumziko la milele. Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…