Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
PICHA MBILI ZA WAASISI 17 WA TANU MWAKA WA 1954
Kuna picha mbili za waasisi 17 wa chama cha TANU tarehe 17 Julai 1954.
Picha ya kwanza ambao hawaonekani katika picha ni ni Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Joseph Kasella Bantu.
Ukitazama picha hiyo ya kwanza hapo chini utaona kuwa kuna maelezo kuwa wazalendo hao hawapo kwenye picha.
Kwa nini hawapo katika picha ni kwa sababu hawa walikuwa watumishi wa serikali na wangetiwa matatani hata kupelekea kufukuzwa kazi endapo serikali ingekuwa na ushahidi kuwa wamehusika katika kuasisisi chama cha siasa.
Kuna picha ya pili ambayo kuna sura ya Kasella Bantu imeingizwa katikati ya Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz.
Kazi hii ilifanywa na Idara ya Picha ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Sijui nini sababu na makusudio ya kufanya hivi kwa kuingiza picha ya Kasella Bantu kwenye picha hii halisi wala sijui kwa nini hawakuweka na picha ya Ally Sykes na Tewa Said Tewa ikiwa palikuwa na haja ya kuweka waasisi wote wa TANU katika picha hii ya kwanza.
Hiki ni kitendawili ambacho bado hakijateguliwa sasa mwaka wa 66 toka TANU iundwe.
Picha hii halisi yaani ''original,'' nimeipiga kutoka kitabu cha Saadan Abdu Kandoro, ''Mwito wa Uhuru,'' (1961).