Picha: Mwisho Mwampamba na mkewe wapata mtoto wa pili

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440


Mtangazaji wa kipindi cha ‘Boys Boys’ cha TV 1, Mwisho Mwampamba na mkewe Meryl ambaye walikutana na kuanzisha mahusiano kwenye Big Brother Africa ‘All stars’, wamefanikiwa kupata mtoto wao wa pili kama couple.

Meryl ambaye ni Mnamibia amejifungua mtoto wa kiume mwishoni mwa May 2014 ambaye wamemuita ‘King David’.
Meryl akiwa na mtoto wa Mwisho (King David) Mwisho na Meryl ambao walifunga ndoa mwaka 2011 walifanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kike 2012.

Couple hiyo sasa ina jumla ya watoto wanne,wawili waliowapata kwenye ndoa na wawili waliowapata kabla ya kukutana, mmoja wa Meryl na mmoja wa mwisho.

Cha kufurahisha zaidi katika familia hiyo ni majina ambayo ambayo wamewapa watoto wao waili,mmoja anaitwa ‘Monkey’ na mwingine anaitwa‘Happy feet’ ambaye ndio mtoto wa kwanza kuzaa na Mwampamba.
 
couple za wazungu hizo! mwanangu bora nimuite mke jina" lakini sio monkey hahahaha
 
Mi nilikuwa najua mwisho ni wa hovyo lakini sio mpaka kwenye maswala ya msingi,hivi unamuitaje mtoto wako MONKEY?
Wazungu wakituita tumbili na kututupia ndizi tunakasirika wakati wenyewe tunajiita Tumbili...
 
ilo jina la Monkey litamletea matatizo mtoto baadaye na atajutia sana.

Ahaha hahaha, labda kwa ki kwao uko lina maana nyingine nzuri tofauti na maana tunayoijua sie

Happy to see you here again bro, karibu tena jukwaani
 
jamani mbona kuna kina simba, tembo, komba, nyati, sungura na mengine mengi au nyani hastahili?
 
Dah!Huyo mtoto akija kukua atawalaani we waache tu,ndo jina gani hilo sasa?Kwa hiyo kibongobongo mwisho anaitwa 'baba nyani' basi sawa!!!!
 
Duh
Hongera zao.

Masikini Ray C ali chezea nafasi hyo saivi yy ndo angekuwa mama mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…