Picha: Nairobi CBD yasalia mahame siku ya maandamano

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Raia wengi wa Kenya hasa wanaofanya kazi kati kati ya Jiji la Nairobi hawajafika mjini kutokana na woga wa vurumai za waandamanaji na mabomu ya machozi.

Maafisa wa polisi wameshika doria katika Barabara nyingi za kati kati ya Jiji. Ikumbukwe Rais William Ruto anatarajia wageni kadhaa wiki hii, wa kwanza akiwa ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres ambaye atarajiwa kuwasili Nairobi Leo.

Aidha pia Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida anatarajiwa kuwasili Nairobi baadae.
Kiongozi mwengine anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Kenya wiki hii ni Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.

Hatahivyo Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amesisitiza kuwa maandamano yataendelea kama kawaida akiwataka wafuasi wake kuandamana mpaka Ikulu.

Tayari maandamano yameanza katika Barabara ya Ngong ambapo basi la usafiri wa umma limeteketezwa na waandamanaji.

Wataalam wengi wa masuala ya kiusalama wamesema kuwa Jeshi la Polisi litatumia mbinu zile zile walizotumia mwezi Jana, ambapo lengo kuu lilikuwa ni kumzuia Odinga dhidi ya kuingia kati kati ya Jiji.
Your browser is not able to display this video.
 
Mwanamke mjinga na mwanaume mjinga watazivunja ndoa zao kwa mikono yao wenyewe." It goes the Sudan way"

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Kitendawili hataniii
 
Hiyo njia ya kutokwenda kwenye shuguli za kila siku ni maandamano ya kimantiki raia wanafanya.

Mtu mwenye akili timamu hapo anatakiwa kulegeza gidani zake, coz uchumi unadorola sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…