Picha: Ni aina gani ya Mbegu za Mahindi ambayo inazaa na kubeba Watoto wengi Kiasi hiki?

Picha: Ni aina gani ya Mbegu za Mahindi ambayo inazaa na kubeba Watoto wengi Kiasi hiki?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kwa wakulima wa mahindi ,Je Kuna mtu anaweza tuambia aina ya mbegu inayozaa Watoto wengi Kiasi hiki au ni Photoshop?
Screenshot_20231026-031658_1.jpg
 
Mkuu mbegu nyingi sana zinazaa vizuri sana mchawi ni aridhi bora au mbolea na maji na utunzaji shamba/palizi kwa wakati

Shamba kama ni kimeo hakuna namna mmea unaweza kubeba mahindi mazuri, hata kama ni jamii ya kubeba pacha kama aridhi ni dhaifu na mvua hafifu itabeba indi dhaifu
 
ardhi yenye rutuba, mvua/maji ya kutosha, kupanda kipindi sahihi cha mwaka, palizi kwa wakati sahihi, mbolea ya viwandani kidogo kwa ajili ya kuboost ile mbolea ya asili, dawa kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu, hvo ndo mchawi wa kupata indi lililoshiba, nyingine mbwembwe tu
 
Mimi sijui ndio maana nauliza
Katika mahindi tunaangalia mbegu yenye uvumilivu wa changamoto na ukinzani wa magonjwa kisha kuzaa sana mwisho gunzi linakuwa na ukubwa au urefu na punje nyingi.
Unapotaka kuvuna mahindi mengi utaangalia hizo sifa.

Mwishi mahindi hutolewa mbegu zake kwa kutegemea Kanda au umbali toka usawa wa bahari,yaani Kanda ya chini,kati na juu.

Kampuni ziko nyingi za mbegu mfano Seedco,Pannar,Dk,Uyole,Zamseed nk...

Mkoa ulipo upewe jibu sahihi maana mvua hazijachanganya,taja mapema
 
Mdomoni Kwa kuona picha kinalipa ila kwenye uhalisia Sasa ndio Utajua hujui.
Kwa kweli. Msimu wa tano huu nimejikita katika kilimo, bado nachechemea. Ninapata hasara kabisa, ila ni kwamba sijakata tamaa.

Kilimo kinacholipa na cha uhakika, labda ni kile cha umwagiliaji. Ila hiki cha kutegemea mvua..sijui. Ngoja tuendelee kujitafuta.

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni nini Hadi upate hasara? Uko Mkoa gani?
 
Back
Top Bottom