Mwalupale
JF-Expert Member
- Apr 29, 2012
- 1,049
- 674
Mpaka sasa (inaelekewa wiki 4) kuna wanafunzi wa baadhi ya vyuo vikuu hapa nchini hawajapata pesa yao ya field (mafunzo kwa vitendo) kutoka loan board kinyume kabisa na mkataba wao na bodi hiyo unavyosema. Wanafunzi wanaishi kwa tabu sana huko waliko kiasi kwamba hawafanyi mafunzo hayo kwa ufanisi. Wasiwasi wangu hasa ni kwa hawa walimu vijana ambao wako mashuleni wanafundisha (field). Kwa wale ambao hawajapata pesa hii sidhani kama watafundisha kwa moyo na kwa wito thabiti. Nilipoona picha hii hapa chini kwenye mtandao flani wa kijamii nilicheka sana lakini nimekuja kugundua kuwa huu ni ujumbe kwa serikali kuwa isitegemee matokeo mazuri na maendeleo ya elimu hapa nchini kama itaendekeza uzembe wa namna hii kwenye mambo makini na yasiyohitaji siasa. Najaribu kufikiria serikali inakosaje pesa kwajiri ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaotegemea kusoma kwa mkopo? Nachelea kusema kwamba kama serikali itaendelea kuleta siasa kwenye mambo makini namna hii basi itambue kwamba inaunda bomu kubwa sana ambalo likilipuka nchi hii haitaitwa kisiwa cha amani tena. Najua wengi watakuja na hoja nyepesi za "wanafunzi wa chuo wana matumizi mabovu ya pesa zao za boom, mara wanashinda bar au wanashinda kwenye kumbi za starehe",: Ninachoweza kusema ni kwamba hiyo sio sababu ya kucheleweshewa pesa yao na kutokupewa kwa wakati kwasababu matumizi ni hulka ya mtu binafsi.
Serikali iwahurumie hawa vijana kwa kuwapatia pesa zao mapema ili wafanye kazi kwa ufanisi kwenye mafunzo yao! Wanatia huruma sana hawa vijana. Madeni yamekuwa makubwa kwa mamantilie walikodhaminiwa kula chakula kwa mategemeo ya kulipa pesa hiyo boom likitoka. Wengine wameshakopa pesa kwa watu mara mbilimbili kwa kutegemea bum. Serikali haijawahi kuchelewesha pesa za posho za wabunge na vigogo, pesa za chai maofisini, pesa za semina na vikao uchwara, pesa za safari zisizo na tija, pesa za mafuta ya magari ya wabunge na pia pesa za ruzuku za vyama! Najiuliza wanafunzi wana makosa gani hadi wacheleweshewe haki zao? Je serikali inatengeneza wasomi wa namna gani kwa mtindo huu? What a bummer!!