Pre GE2025 Picha: Tume Huru ya Uchaguzi yatinga mtaa kwa mtaa mkoani Morogoro kuhamasisha wananchi kujiandikisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Huko mkoani Morogoro, wafanyakazi wa Tume Huru ya Uchaguzi wameanza kuingia mtaani na kuandaa events ndogo ndogo kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na kuhamasisha wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

Haya ndio mambo tunayotaka kuona.

Sasa hapa tume ingepiga na Insta Ads na partnerships na online media wangetisha zaidi, maana vijana wengi ndo wanashinda huko mitandaoni.

==========================================
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 22 Februari, 2025 imetoa Elimu ya Mpiga Kura kutumia Gari la Elimu ya Mpiga Kura kwenye Mnada wa Rubeho uliopo Kata ya Rubeho Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro na kuwahamasisha wakazi wa halmashauri hiyo kwenda kujiandikisha au kuboresha taarifa zao wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kuanza tarehe 01 hadi 07 Machi, 2025 katika Mkoa wa Morogoro na baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Tanga.





 
Dah, ila raia tumechoka jamani. Embu tutazame kwenye hiyo picha ya kwanza, yaani kama tupo vitani tofauti na hao waliosimama majukwaani, sura zina nuru.
Hapo sio kivu mashariki kweli?
 
Wanahamasisha nini wakati viongozi wameshatuchagulia?
 
Siyo wanajinadi wenyewe kweli? Mbona vidoleni hakuna kinachong'aa
 
Tuwe tu wakweli. Tanzania hatuna Tume Huru ya Uchaguzi! Kilichobadilika hapo ni jina tu. Ila tume ya uchaguzi ni ile ile Tumeccm.
 
Jina ni tume huru, matendo na sheria zina akisi huo uhuru wa hiyo tume
 
well done NEC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…