nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
Uwanja wa taifa wa zamani ambao kwa sasa unajulikana kama uwanja wa Uhuru au shamba la bibi, umefungwa kwa muda mrefu ili kupisha ukarabati wa uwanja huo, kwa muda mrefu uwanja wa Uhuru tumekuwa tukiona ukitumika kwa shughuli za kitaifa kama siku ya Uhuru na nyinginezo, bado mafundi wanaendelea na ukarabati.
Huenda ukawa hujabahatika kupata nafasi ya kuona maendeleo ya uwanja huo kwa hizi siku za karibuni toka ufungwe, ripota wa millardayo.com nilipata nafasi ya kukupigia picha 29 za ukarabati ulipofikia. Kwa asilimia kubwa sehemu iliyofanyiwa matengenezo ni majukwaa ya mzunguuko ambayo awali yalikuwa na vyuma, na juu hayakuwa na paa.
Hii ni sehemu ya VIP ambayo ipo kama ilivyokuwa awali
Muonekano wa majukwaa ambayo kabla ya ukarabati yalikuwa na bomba za chuma kama jukwaa ila sasa wameboresha.
Muonekano wake ukiwa katika ngazi za uwanja wa Taifa
Hivi ni vyoo vya zamani lakini bado havijafanyiwa ukarabati ujenzi bado unaendelea
Sehemu ya nyuma ya kuingilia katika jukwaa la VIP
Muonekano wa majukwaa kwa nje nyuma
Sehemu ya kuchezea ambayo bado ina nyasi bandia za awali
Wasaidizi wa wachina katika ujenzi wa uwanja huo ambao bado wanaendelea na kufyatua tofali.
Sehemu ya VIP pamoja na njia ya kuingilia magari na kutokea Uwanjani.
Sehemu ambayo mafundi wanahifadhia vifaa vyao vya ujenzi
Fundi akisomba kokoto za kuchanganyia zege gari
Hii ni njia ya kupitia magari
Sehemu inayoonekana kama mashimo ni ngazi za kutokea na kuingilia sehemu yalipo majukwaa.
Ngazi za kuingilia katika majukwaa kwa nje
Namna ya ngazi zilivyo lazima uzunguuke mara moja kabla ya kufika Jukwaani
Njia ya kutokea gari