Picha: Vita ya Ray C na Zamaradi yapamba moto

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Wale Mastaa waliodaiwa kuingia kwenye bifu zito, Zamaradi pamoja na Ray C, na baadae kupatana, huku chanzo cha bifu kikidaiwa kuwa ni mwanaume, bifu hilo limeibuka tena, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni maneno ya kejeli ya mtangazaji zamaradi mketema kwa mwanamuziki Ray C.

Hivi karibuni Zamaradi alipost picha ya mwanae kwenye mtandao wa Instagram akim wish Happy birthday, uku aki repost baadhi ya pongezi kutoka kwa baadhi ya mastaa na mashabiki mbali mbali wa mtangazaji huyo, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuwa mwiba kwa mwanamuziki Ray C ambaye mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto.

Mtangazaji huyo ambaye baadae tena aliandika comment kwenye page yake, akiwauliza mashabiki wake ni kitu gani ambacho wanatamani kuwa nacho katika maisha lakini hawana? Au wengine wanavyo na vinawafanya wawe na furaha?

Comment hiyo ilizua utata uku baadhi ya wadau wakidai lile lilikuwa dongo kwa hasimu wake wa mda mrefu ray c ambaye mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto wala kuolewa, ndipo team Ray C ilipoamua kumtag boss wao huyo ambapo Ray C hakutaka kulaza damu na kuamua kujibu mapigo kwa mtindo ule ule wa vijembe, hali iliyozua balaa uko Instagram na kuziacha team hizo mbili zikishambuliana kwa matusi ya nguoni.

Ray C baada ya kuona hali inakuwa mbaya, alihoji kama Zamaradi ndiye mwanamke pekee aliyezalishwa bila kuolewa apa duniani? Aliwataka watu waache kuhisi vitu ambavyo hawana uhakika navyo. Mpaka sasa bado Zamaradi hajazungumza chochote kuhusu varangati hilo.

Chanzo: Instagram

Written by warumi
 

Attachments

  • 1427007006391.jpg
    57.5 KB · Views: 7,326
Hem ngoja kwanza!
hii piccha ray c angepiga bra angetoka msupuuuu!!iiiiila saaaaasa duh"!
 
Ninacho jiuliza kwanini Rayc ahisi anaambiwa yeye? Mbona kuna mastaa wengi hawana watoto na hawaja jihisi? Kwanini Wema au jokate,Walper hawakuhisi wanasemwa wao? Nimegundua Rayc bado anaugua kabisa!
Rayc ni attention seeker kabisa na anapenda ugomvi!
 

Ha ha ha lazima ajihisi yeye maana wameshare bwana.Hao wote wamekutana huyo zamaradi nae anajiona kaukata sana.
 
ni kweli Ruttashobolwa...but ako ka Zamaradi nako hujiona kapo juu, yani ana maneno meeeengi mi ananikera kwakweli! uyo Ray C mnyalu mwenzangu ngada haijaisha yote kichwani
Hapo kwenye green hilo ndilo tatizo linalo mkabili Rayc..
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha lazima ajihisi yeye maana wameshare bwana.Hao wote wamekutana huyo zamaradi nae anajiona kaukata sana.

Duu hatari sana..kwanini na yeye asitafute mtoto?Kujibishana insta kutamsaidia kubeba mimba?
 

Kwa sababu wana share bwana, ila yeye hakubahatika kuzaa naye ndio maana anajihisi yeye ndiye mlengwa
 
Hahahaaa, Uwiiiiii!

Na yeye ana mimba nini maana huo mkao.. ila kanichekesha eti bitches be like im pregnant again, ahahahah hlo dongo ni la zamaradi kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…