Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Ukishaanza kuona picha kama hizi ujue kabisa Uchaguzi umekaribia.
Hawa ni moja watu watakaoenda kuamua nani ataenda kuwa diwani, Mbunge au Rais wako.
Wasiende tu kurudia yale mambo tuliyoayaona kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
=============================================
Washiriki wa mafunzo ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Mkoani Tanga wakila kiapo kabla ya kuanza kwa mafunzo yao ya siku mbili leo tarehe 10 Februari, 2025.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Mkoa wa Tanga katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza sambamba na Mkoa wa Pwani kuanzia Februari 13 hadi 19,2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.