Picha: Watu wawili wanaofanana na Rais Rodrigo Duterte na Rais Kim Jong-un wazua vioja Hong Kong

BuletAngle

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2017
Posts
688
Reaction score
556


Huenda ukadhania kwamba rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walikuwa pamoja katika barabara za mji wa Hong Kong, wakipiga picha na kula pamoja chakula cha jioni katika mgahawa mmoja.

Lakini uchunguzi wa kina ulibaini kwamba wawili hao walikuwa watu waliowaiga viongozi hao wawili.
Kutana na jamaa anayejiita Cresencio Extreme anayefanana na Durtete na Howard X anayefanana na Kim Jong un.



Wawili hao waliobeba bunduki bandia walisalimiwa na wafanyikazi na raia walipowasili katika mgahawa huo wa kuku karanga au Fried Chicken Restaurant



Walihudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la St Joseph's huku Cresencio Extreme (kushoto)akiwa amevalia shati jeupe ambalo hupendwa sana na rais Durtete



Mtu huyo anayefanana na rais Durtete alizua kihoja na mkanganyiko katika kanisa hilo katikati ya mji wa Hong Kong baada ya kuzungukwa na waumini



Je huyu ni Durtete?'' Wengine hawakukubaliana naye huku raia huyo akionekana kuwa mdogo kwa umri kuwa rais wa Ufilipino pamoja na mwenzake anayemuiga rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.



Wawili hao walizidi kuwakanganya raia waliopoonekana wakila chakula cha jioni katika mgahawa wa Hong Kong siku ya Jumapili.


Mr Duterte {kushoto) na muigaji wake


Bwana Kim (kushoto) na muigaji .
 
Kuna movie inaitwa the interview ya mshkaji wa kuitwa Ellen lapapoul na Devin skylock wanaenda kumuhoji Kim. Nadhani huyo jamaa angejitokeza kabla wangemchukua ni copy right kuliko aliyetumika mule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…