warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
UNAFIKI 100 % ! Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ' Kay' , ameibua mshangao baada ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ' Madam' ambaye kwa sasa haziivi na Kay .
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI
Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema , Aunty Ezekiel Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio , Masaki jijini Dar .
WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo , alimkuta Wolper akila raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa ' wamemisiana' . Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa wakinong ' onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minong ' ono ikaanza .
WATAALAM WA UBUYU
Kitendo cha Wema kutumia dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper , kilitafsiriwa na wataalam au wafuatiliaji wa mambo ya watu ( ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema . Wema Sepetu akimha gi Jacqueline Wolper. "Mh! Mwenzangu makubwa, huyu Wolper si ni Timu Kajala ? Inakuwaje anatoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa adui wa Kajala ? Hapa kuna tatizo, unafiki kwa mastaa kamwe hauwezi kuisha , " alisikika mtoa ubuyu mmoja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.
AKUMBUSHA VITA YAO
Kama hiyo haitoshi , mtoa ubuyu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema , ukiachilia mbali Wolper kuwa karibu na Kajala lakini hata yeye ( Wolper ) alikuwa kwenye vita nzito na Wema kwa kudaiwa ' kushea ' naye penzi la msanii Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz ' . "Wolper jamani mnafiki. ..si ndiyo huyuhuyu aliwahi kuingia kwenye vita nzito na Wema baada ya kudaiwa kuwa anadondoka dhambini na kipenzi cha Madam, Diamond ? Yaani huu ni unafiki asilimia mia ," alisema mtoa ubuyu huyo.
TIMU KAJALA WAJA JUU
Baada ya Timu Kajala kusikia kwamba Wolper ' ali - spendi ' vya kutosha na Madam kwenye bethidei hiyo , walikuja juu kisha wakamtolea uvivu na kuanza kumshambulia katika mitandao ya kijamii na kudai hafai kuwa timu yao. Huku wakati huo huo. .. Jacqueline Wolper "Wolper msaliti , ataendaje kwenye sherehe ya mpinzani wetu? Tena kama hiyo haitoshi , yeye anakumbatiana na Madam ambaye kwetu sisi hatusaidii lolote, " alisema mmoja wa Timu Kajala .
KUMBUKUMBU IPOJE ?
Kabla ya siku hiyo , Wolper na Wema hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na kila sehemu ambayo utakumta Wolper , kamwe huwezi kuona Wema ametia maguu .
WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya paparazi wetu kushuhudia kitendo hicho ukumbini , alimfuata Wolper na kumuuliza ni kitu gani kilichowasababisha wapatane na kuoneshana ' mahaba niue ' wakati nyuma ya pazia wana bifu ? Msikie alichojibu :
"Ujue watu wengi sana wamekuwa wakidhani mimi na Wema tuna bifu , sijui kwa kuwa mimi nina ukaribu na Kajala au kwa kuwa hatujawahi kuwa pamoja , lakini ukweli mimi na Wema siyo waongeaji sana japokuwa huwa nikiweka picha au chochote kwenye Instagram, Wema huwa ana- like na mimi huwa na- like vitu vyake hivyo sidhani kama nilikuwa na tatizo naye sana, " alisema Wolper .