Picha ya Ally Sykes Badala ya Abbas Sykes Picha ya Said Chamwenyewe ''Hajulikani''

Picha ya Ally Sykes Badala ya Abbas Sykes Picha ya Said Chamwenyewe ''Hajulikani''

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA YA ALLY SYKES BADALA YA ABBAS SYKES PICHA YA SAID CHAMWENYEWE ''HAJULIKANI.''

Siku moja nadhani katika miaka ya 1980 nimemtembelea Ally Sykes ofisini kwake akaitisha file kutoka kwa katibu muhtasi wake Bi. Zainab.

Bwana Ally ni mtu wa maskhara sana huyu dada yangu alipokuja kuomba kazi kwa Bwana Ally kazi alipata lakini akamwambia, ''Itabidi hapa nikubadilishe jina wewe Zainab na mke wangu Zainab sasa wewe ukiwa huko nje utakuwa Zainab lakini hapa ofisini kwangu mimi nitakuita ''Chausikiu.''

Yale yalikuwa maskhara tu jina lake lilibakia lile lile alilopewa na baba yake - Zainab.

Basi lilipokuja file alilolitaka akafungua akatoa ''cutting'' ya Daily News ya picha ya Said Chamwenyewe.

Caption ilikuwa inasema mzee huyo kwenye picha hajulikani.

Ally Sykes akatingisha kichwa ka masikitiko.

Leo katika gazeti moja kuna TOLEO MAALUMU LA NYERERE ndani kuna makala, ''Simulizi ya Balozi Sykes na Jeneza la Mwalimu Nyerere.''

Picha iliyowekwa kuendana na makala haya ni picha ya Ally Sykes badala ya Balozi Abbas Sykes.

Siku ile alipokuwa ananionyesha cutting ya Daily News iliyokuwa na picha ya ''mzee asiyejulikana,'' Ally Sykes kwa masikitiko alinambia, ''Mohamed itafika wakati sisi sote tutakuwa hatujulikani na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika itabakia ya Nyerere peke yake wewe subiri tu utakuja kuona.''

Leo nilipokuja kuona Abbas Sykes mtumishi wa serikali wa miaka mingi akiwa balozi na mtu maarufu sura yake haijulikani inachanganywa na ya kaka yake nikamkumbuka sana Bwana Ally na utabiri wake.

Mwaka jana kulikuwa na makala katika gazeti moja, makala hiyo ilikuwa ni kumbukumbuka ya miaka 50 ya kifo cha Abdul Sykes.

Picha iliyowekwa ilikuwa ya Hamza Mwapachu badala ya Abdul Sykes.

Nani huyu Said Chamwenyewe?

Julius Nyerere alipokwenda kuisajili TANU Waingereza wakamuuliza kama ana ''register book,'' ya wanachama.

Mwalimu hakuwanayo.

Kisa hiki kanihadithia Bi. Zainab mbele ya mumewe Bwana Ally.

Bi. Zainab anasema, ''Tulikuwa sote nyumba ya Kipata tunamsubiri Nyerere aje atupe taarifa, mimi Bwana Ally na Bwana Abdul katoka kwake Stanley yuko pale nyakati za mchana tunamsubiri Nyerere.

Nyerere kuingia tu akazama kwenye sofa kanyongea akatuambia kuwa Msajili amekataa kuisajili TANU kwa kuwa hatuna ''register,'' ya wanachama.

Abdul Sykes akatoa amri akasema, ''Nitafutieni Mzee Said Chamwenyewe.''

Mzee Said Chamwenyewe alipopatikana Abdul akampa ''register book'' na kadi za TANU akamwambia aende Rufiji akailetee TANU wanachama.

Mzee Said Chamwenyewe alipopatikana Abdul akampa ''register book'' na kadi za TANU akamwambia aende Rufiji akailetee TANU wanachama.

Said Chamwenyewe alisafiri kwa baiskeli kutoka Dar es Salaam hadi Rufiji na aliporudi akamkabidhi Abdul Sykes ''register'' ya wanachama na fedha za mauzo ya kadi akazipeleka kwa Iddi Faiz Mafungo, Mweka Hazina wa TANU.

Kuna mengi ningeweza kueleza kuhusu Said Chamwenyewe lakini tusimame hapa.

Nitakileta kisa kingine nini kilitokea alipofariki Iddi Faiz Mafungo.

Katika picha Said Chamwenyewe ni huyo wa nne waliosimama kulia baada ya Jumbe Tambaza,
 

Attachments

  • ALLY SYKES BADALA YA ABBAS SYKES.jpg
    ALLY SYKES BADALA YA ABBAS SYKES.jpg
    11.6 KB · Views: 3
  • BARAZA LA WAZEE WA TANU.jpg
    BARAZA LA WAZEE WA TANU.jpg
    36.8 KB · Views: 4
  • HAMZA MWAPACHU NA ABDUL SYKES.png
    HAMZA MWAPACHU NA ABDUL SYKES.png
    24.8 KB · Views: 3
Iko muzuri sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Siku ile alipokuwa ananionyesha cutting ya Daily News iliyokuwa na picha ya ''mzee asiyejulikana,'' Ally Sykes kwa masikitiko alinambia, ''Mohamed itafika wakati sisi sote tutakuwa hatujulikani na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika itabakia ya Nyerere peke yake wewe subiri tu utakuja kuona.''

Ndugu Mzee Said, ni nini ulijiuliza wewe baada ya Mzee Ally kutamka maneno hayo?

Je ina maana hakuwa hata na imani kwako kwamba utaweza kurekebisha upungufu huo?

Kama kuna jambo linakosewa ni nani anapaswa kuwajibika, na nani anapaswa kumuwajibisha mkoseaji?

Na je kati ya wale taarifa zao zinaokosekana ni kina Sykes brothers pekee yao?

Mimi nadhani badala ya wewe pia kuendeleza lawama, ungepambana kueleza kila unachojua kuhusu Wazee wako hao, na vivyo hivyo watatokea wengine watawasema ya Wazee wa kwao.
 
Back
Top Bottom