Picha ya Dr. Bushiri Tamim Daily News Mgomo wa Madaktari

Picha ya Dr. Bushiri Tamim Daily News Mgomo wa Madaktari

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
DR. BUSHIRI TAMIM PICHA MBELE YA DAILY NEWS YUKO KAZINI MADAKTARI WENZAKE WAKO KATIKA MGOMO

Nilikuwa nimefadhaika sana kwa kukosa picha ya Daily News ikimuonyesha Dr. Tamim akiwa kazini wakati madaktari wenzake wamo katika mgomo.

Nilikusudia kuweka picha hii kwenye taazia yake na nilipoikosa nilisikitika sana.

Ndipo nikaamua kuweka picha ya yake kakaa kwenye kizingiti cha mlango wa kuingia Msikiti wa Makonde.

Yote haya mipango ya Allah.

Leo usiku huu naingia maktaba kutafuta picha ya Ustadh Masudi Adam sijaipata naiona picha ya Dr. Tamim ya tarehe 25 January 2012 picha ambayo nimehangaika kwa siku mbili kuitafuta.

Picha imenijia bila ya hata kuitafuta.
Picha imenizukia.

Ustadh Masudi Adam ni msomaji Qur'an Bingwa karithi kwa kwa baba yake Sheikh Adam aliyekuwa Bingwa wakati wake.

Kisa ya haya yote Balozi Dau kanirushia audio Ustadh Masudi anaongea na baba yake kutokea Uingereza wanamzungumza Dr. Tamim.

Masudi alipokuwa mchanga aliumwa sana.

Ustadh Masudi anamwambia baba yake Sheikh Adam kuwa Dr. Tamim akimuona anamwambia, ''Masudi njoo unisomee Qur'an nifurahi unilipe kwani nimekutibia sana ulivyokuwa mtoto.''

Nilipomaliza kusikiliza mazungumzo haya kati ya Sheikh Adam na Ustadh Masudi na kwa hakika mazungumzo ya kupendeza kuhusu nikawa nimepata kitu cha kuandika.

Haraka nikaingia Maktaba kutafuta picha ya Ustadh Masudi.
Haikuja picha ya Ustadh Masudi imekuja picha ya Dr. Tamim.

Roho ikanipiga "Paa," kuona uso wa Dr. Tamim mbele yangu.

Hakika Allah ni mwingi wa rehma.
Furaha yangu haielezeki.

Huu kwangu ni muujiza.

Picha nimekuwekeeni nanyi mstafidi mumuuone Daktari Mzalendo Bushiri Tamim siku ya mgomo akiwa kazini kuwatibia wagonjwa.

Dr. Tamim anastahili nishani kwa uzalendo wake kwa kukataa kugoma akawa kazini kuwatibu wagonjwa masikini wasiokuwa na uwezo wa kwenda hospitali za kulipia.

Kuna awezae leo kukisia thamani ya utu, ubinadamu, uzalendo na moyo wa huruma wa Dr. Bushiri Salum Tamim?

Yupo awezae kuweka katika mizani ubinadamu huu wa daktari kumkimbilia mgonjwa masikini asiye na pa kushika akamfariji?

Yupo?
Tuna deni kubwa kwa Dr. Tamim.

Hatukumlipa wala kumuadhimisha katika uhai wake basi tumlipe leo akiwa kaburini.

Tusiwe wezi wa fadhila.
Malipo ya hisani ni hisani.

1716147490584.png

Dr. Bushiri Salum Tamim

 
Back
Top Bottom