Picha ya mmiliki wa home shopping center


MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hali yake inadaiwa kuendelea vizuri, lakini kuna uwezekano wa jicho lake moja kutokuona kabisa baada ya kuathirika sana, lakini jicho la pili liko salama.
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.



HII NDIYO TINDIKALI YENYEWE (SULPHURIC ACID) >>> ANGALIA VIDEO UONE NAMNA GANI ILIVYO HATARI




 
Last edited by a moderator:
Pole mkuu......ila ka ulidhulum haki yako....
 
Ziko wapi jeuri zote?
Ujafa hujaumbika, Labda akirudi atakuja kutubu madhambi yote aliyowafanyia wafanyakazi wake na watu wengine.
 
Pole sana! Mungu akujalie upone mapema na wahalifu hawa wajulikane haraka iwezekanavyo na waweze kukumbana na vyombo vya sheria.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ila kwa kuwa wewe sio mpiga makelele humu kama mcdm ela itakubadilisha na utakuwa nomol soon
 
mbona sehemu kubwa hivyo inaonekena huyo mchizi alikuwa ameibeba kwa beseni, ni dhuluma au kesi ya mke wa mtu mwenye mawivu ya kuua.
 
Dah apone haraka inshaAllah.. i hope waliofanya hivi watakamatwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…