Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Mji mmoja hivi wa bandari kutoka Kaskazini Mashariki mwa England, ndio mji huu unaomiliki binadamu vichaa zaidi wa soka duniani.
Wenyewe hupenda kujiita 'The mighty Reds' yaani wababe wekundu. Sorry! Naizungumzia Liverpool inayoshabikiwa na Lebron James, Nelson Mandela, Ali Kiba and of course Mzee Muchacho[emoji847].
Kuna sifa moja ya pekee inayowatenganisha binadamu wa Liverpool na mashabiki wa timu zingine zote duniani. Ni sifa gani hiyo?? UKICHAA. Naam, nauzungumzia ukichaa huu-huu unaotibiwa kule makao makuu ya nchi.
Ni binadamu hawa ambao wakipiga goma lao la You'll Never walk alone wanasahau hadi majina yao ya ubatizo, wanasahau na kujitambulisha kama Liverpool.
Ni binadamu hawa ambao wakishakata kilaji vizuri, walewe chakari kisha wapige dude la 'Fields of Anfield Road' wanajihisi wamesimama katikati ya Uhai na kifo, hakuna cha maana tena mbele yao zaidi ya Liverpool.
Ni binadamu hawa ambao wakishaingia Anfield wanasahau taaluma zao, wanasahau vyeo vyao na wanasahau utajiri wao na wote wanakuwa kitu kimoja. Daktari anajipaka rangi nyekundu kama konda wa daladala na tajiri anabeba bango la 'This is Liverpool'
Ni binadamu hawa wa Liverpool ambao hata wawe nyuma kwa mabao matatu na zimebaki sekunde tu mechi kumalizika bado watakuwa na nguvu ya kushangilia kama wanaongoza kwa mabao mengi au kama vile wana dakika 90 zingine za kusawazisha.
Ni binadamu hawa ambao wapo tayari kukanyaga maili za kutosha kwa ajili tu ya kuisapoti Liverpool. Wapo tayari kuacha shughuli zao kwa ajili ya Liverpool. Wapo tayari kisafiri kwa anga, maji au ardhi lakini tu walisapoti chama lao.
Hii ndio sifa za watu wa Liverpool. Iwe jua, iwe mvua, Maisha yao ni Liverpool.
Hizi ni sifa za watu wa Liverpool lakini kwa leo zibadilishe kisha useme hizi ni sifa za watu wa Simba.