- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam Wakuu,
Nimekutana na picha ya ndege iliyopata ajali kwenye mtandao wa X ikidai ni ndege iiyopotea iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Rais wa Malawi.
Je ni kweli picha na taarifa hiyo ni sahihi?
Nimekutana na picha ya ndege iliyopata ajali kwenye mtandao wa X ikidai ni ndege iiyopotea iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Rais wa Malawi.
Je ni kweli picha na taarifa hiyo ni sahihi?
- Tunachokijua
- Mnamo Juni 10, 2024 nchi ya Malawi ilikumbwa na taarifa nzito iliyoripoti kupotea kwa ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa nchi hiyo Saulos Chilima na Maafisa wengine 9 (Soma hapa).
Leo Juni 11, 2024 kupitia mtandao wa X kumzuka picha yenye taarifa inayodai ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima imepatikana na huku watu wote Makamu na Maafisa tisa waliokuwepo wamefariki. Sehemu ya taarifa hiyo inasema:
Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima na wengine 9 wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya ndege. Ndege imepatikana na wote 10 waliokuwa ndani wamefariki!Je, kuna ukweli kuhusu taarifa na picha hiyo?JamiiCheck imefanya ufuatiliaji picha na taarifa iliyoambana nayo na kubaini kuwa haina ukweli. Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Google Reverce Search umepata matokeo yaliyoonesha kuwa picha ya ndege iliyopata ajali inayohusishwa na tukio la kupotea kwa ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi ipo mtandaoni tangu Septemba 26, 2020. Picha hiyo ilieleza tukio la ajali ya ndege ya kivita ya Ukraine iitwayo An-26 (taarifa yake soma hapa).
Picha ikionesha habari iliyoripoti ajali ya ndege ya kijeshi ya Ukraine September 26, 2020
Zaidi ya hayo JamiiCheck imefuatilia vyanzo mbalimbali kupata sasisho la kupotea kwa ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima na maofisa wengine 9 lakini mpaka sasa hivi saa 5:30 asubuhi ya Juni 11, 2024 hakuna taarifa yoyote kutoka vyanzo rasmi iliyothibitisha kupatikana kwa ndege hiyo na kufariki kwa Makamu wa Rais na Maofisa wengine 9 waliopotea kwenye ndege.
Mathalani, taarifa ya Rauters ya leo Juni 11, 2024 inaeleza kuwa bado harakati za kuitafuta ndege hiyo zinaendelea (Soma hapa).
Zaidi ya hayo taarifa CNN (hii hapa) inabainisha kuwa bado harakati za kusaka ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi zinaendelea, zoezi hilo linachelewa sababu ya hali mbaya ya hewa. Nalo, Jeshi la Malawi linasema bado linaendelea kuisaka ndege ya Makamu wa Rais, na linawaomba watu waache kusambaza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.
Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa na JamiiCheck tumejiridhisha kuwa taarifa na picha iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikihusisha tukio la kupotea kwa ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi haina ukweli.
Taarifa ya CNN 11:22 (Juni 11, 2024) ikieleza muendelezo wa harakati za kuisaka ndege hiyo