Picha za mpenzi (au wapenzi) wako wa zamani..

duuh nakuelewa ndugu yangu inataka moyo kweli maana unaanza ku imagine mambo mengi ukiona picha ya mtu mwenyewe halisi bora kutomjua kabisa....

mi niliweka kwenye album, mwenyewe alipoziona aliziangalia,akamthaminisha,akaniuliza huy nani? Nilipomwambia ni ma x akazichukua na kuziweka chini ya picha zingine.
 
Hii topi imenigusa sana..
Ngoja nsijibu kitu .......

Sante Amyner
 
Duh,kuwa na mpenzi JF tatizo kweli.
Hapa nashindwa kutoa opinion yangu maana hakuta kalika hapa.
Ngoja nifikirie kuchange ID
 
aisee mi nikitakaga kuzidelete najiulizaga miaka 30 au 40 ijayo ntakumbuka kweli watu niliokuwa nao katika uhusiano huko nyuma?so i keep them as memory for my own meaning.for now zipo ndani ya box ambalo nimeliacha home kwa wazazi na sio kwangu na nimeshampiga biti maza asizitupe
 
Mm huwa nazijaza kwenye bahasha na kuzituma kwa muhusika!!
 
jamani canta kweli ulikuwa na dhumuni la kumsahau totaly! Mpaka zawadi....!!?
Ila kuna wanaume hawapo worth kuwakumbuka even for a second.. Memories huleta pain and heart aches! Picha unaziyeyusha na acid kabisa hata majivu yasibaki...
Huwezi amin mpaka zawadi za nguo niliteketeza kbs,
Na nashukuru iliniwezesha kusahau kbs na kuanza upya maisha bila yeye.
 
nilikua nimehifadhi picha nyingi na kadi za toka kidato cha kwanza
baada ya kwenda chuo semi 1 nilivyorudi home likizo zote zikapikia
kande na mama akafurahi kwani bajeti ya mkaa iliondolewa siku hiyo.
 
Let bygones be so....................tuuuuupaaaaa kuuuuleeeeeeeeee
 
mh! Aisee nikizifuma za wife patachimbika, ila mm ninazo cjui atamaindi akiziona? Maana za kwenye cm naona hamaindi!

kijana matatizo yakitokea usije kuomba msaada hapa nakuona unalea ugonjwa na unafurahia tu!kama umeshahisi ukikuta za mkeo utaumia kwanini ujifariji kwamba mkeo akikuta zako itakuwa poa tu?
 
ishu ni kuzipiga kiberiti tuu,but mm ninayo 1 ya mpenzi wangu wa kwanza kabisa,na siwezi kuichoma moto wala kuipoteza coz girl/ nam-love bado!
 
nizihifadhi kwani mi jumba la makumbusho?za kazi gani for my present and my future?
 
ishu ni kuzipiga kiberiti tuu,but mm ninayo 1 ya mpenzi wangu wa kwanza kabisa,na siwezi kuichoma moto wala kuipoteza coz girl/ nam-love bado!

safi mkuu!endelea kuhifadhi hadi ndani ya ndoa yako!Mungu akikuandalia mwanamke ambaye naye amehifadhi ya mwanaume wake wa kwanza usije kuliakulia hapa!ktk ulimwengu wa kiroho matenda yetu ndio yanayoamua wakati wetu ujao...kaa ukijua hilo
 

Mwenzenu zipo ktk PAKACHA LANGU lenye vitu vya historia chakavu teh!
 
uwekaji wa kumbukumbu unategemeana sana na hisia zako mwenyewe - kama binadamu tunatunza vitu vinavyotufurahisha, kutufundisha, na kujitambua. Picha na vielelezo tu. Kama wawili walitengana kwa amani ama mabadiliko ambayo hayakuweza kuepukika - kuhama, kukua, kutofautiana kindoto nk utupaji wa picha si dharura! Lakini kama ni tafrani ama uhusiano haukuwa na maana yoyote basi utunzaji wa kumbukumbu unakuwa sio muhimu maana hisia au sababu za kuweka kumbukumbu zinakuwa hakuna.
 
Mbona nshaoa kitambo na nna watoto 4 na wife kishaziona hata kabla ya kumchumbia?MAVI YA KALE HAYANUKI MKUU.
 
mi niliweka kwenye album, mwenyewe alipoziona aliziangalia,akamthaminisha,akaniuliza huy nani? Nilipomwambia ni ma x akazichukua na kuziweka chini ya picha zingine.

Mimi zilipotezwa kabisa... Ghafla tu niliona picha fulani zinamiss! Na ni zile nikiwa na akina dada,baadhi lovers,na baaadhi siyo...

Kwa wivu tu zikapotezwa...
 
nilikua nimehifadhi picha nyingi na kadi za toka kidato cha kwanza
baada ya kwenda chuo semi 1 nilivyorudi home likizo zote zikapikia
kande na mama akafurahi kwani bajeti ya mkaa iliondolewa siku hiyo.

hahahaha hii balaa sasa..
 
hahahahaah, wife wako mjanja hapo kakukataza coz anajua naye ana yake wa zamani so ngoma iwe droo ukiichoma tu moto akishtukia huo mchezo ujiandae kipigo kama cha wanaume wa kenya.
 
Hii topi imenigusa sana..
Ngoja nsijibu kitu .......

Sante Amyner

jamani AD tuambie umezifanyeje pics... Usijali wala simwambii kaka.. Najua hapatatosha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…