Picha za Wema akiwa na bwana ake zavuja

Midekoo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
45,757
Reaction score
246,786



Mrembo mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ ameendelea ‘ku-shine’, safari hii zimevuja picha mpya akiwa bafuni na mpenzi wake aitwaye Bakari Kila.

Chanzo makini kilinyetisha kuwa, licha ya Bakari kuwa nyuma ya nondo kwa msala wa madawa ya kulevya Mombasa, nchini Kenya, bado ana ubuyu wa picha mpya za Wema wakioneshana mahaba na mpenzi wake huyo wakiwa bafuni.

“Achana na skendo ya unga inayomtafuna bwana wa Wema, sahau kabisa kuhusu zile picha zilizovuja Wema akiwa na Bakari, mimi ninazo picha nyingine mpya wakiwa bafuni.

“Yani ni full mahaba, Wema anaonekana akiwa ametinga kanga moko (moja), amemkumbatia Bakari huku akimpiga busu motomoto,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kuna moja Wema anambusu Bakari shavuni lakini kuna nyingine anambusu mdomoni kabisa kama njiwa vile tena wakiwa kwenye hisia kali za kimalovee. Madam hana habari tena yeye inaonesha ndiye aliyekuwa anapiga picha.”

Bakari anatajwa kuwa na mkwanja mrefu kiasi cha kumtuliza Wema hadi akaacha ‘makeke’ ya mjini, kabla jamaa huyo hajataitiwa kwa madawa ya kulevya nchini Kenya.
 
Dah....hapo ndipo huwa Napata utata sana kwenye kuelewa....Sijui akili yangu ni nzito....🙁🙁🙁🙄
 
Madawa ya kulevya? Na wema naye kwenye scandal hiyo hiyo? Je, ndiyo yaliyowaleta pamoja?
Nimewaza kimya jamani (sijasema)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…