nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
[h=1]Zanzibar Daima Online[/h][h=2]Jarida la Kila Mzanzibari[/h]
[h=1][/h]khelef / 7 days ago

Na Mwandishi Wetu, Chake Chake, Pemba. Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na bado katika visiwa vya Unguja na Pemba, kumekuwa na dhana kwamba jamii ya Kipemba haikushiriki kuiangusha serikali iliyoundwa na muungano wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP au Hizbu) na Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) tarehe 12 Januari 1964.
Dhana hiyo inapigiwa chapuo sana na viongozi wa kisiasa na hata wa kijamii ndani na nje ya Zanzibar, ambao kwa makusudi au kwa ujinga wa kutokujua wamekuwa wakisaidia kuipasua jamii ya Zanzibar hata leo, nusu karne baada ya Mapinduzi hayo kufanyika.
Hivi karibuni iliripotiwa kwamba jeshi la polisi Zanzibar liliwakamata watu wanaojiita wastaafu wa serikali, wakulima na wakwezi wa Unguja, ambao katika matukio tafauti waliipaza sauti ya kutaka Unguja na Pemba zigaiwe kwa hoja kwamba Wapemba ambao hawakushiriki kwenye Mapinduzi ya 1964, leo hii wamekuwa kimbelembele kutaka kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni mtoto wa Mapinduzi hayo.
Inasemekana kuwa watu hao, wengine wakiwahi kuwa mawaziri na wakuu wa wilaya katika awamu za serikali zilizopita, walihojiwa kwa kipengele cha kuhatarisha usalama na umoja wa nchi. Hata hivyo, tafauti na wengine waliokamatwa kwa shtuma kama hizo, kwa mfano viongozi wa jumuiya ya Uamsho, hawa wastaafu hawakuwekwa ndani wala kufunguliwa kesi yoyote hadi sasa.
Makala haya hayana lengo la kuwazungumzia khasa watu hao, bali yamejikita kisiwani Pemba kwenyewe kwa nia ya kuangalia kwa namna gani sifa hii ya ushujaa wa kujitolea kwa roho na mali ya kupindua serikali visiwani Zanzibar, Mpemba naye inamstahikia.
Mwandishi wa makala haya ameitembelea Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kisiwani Pemba katika jengo linalojulikana kama Old Fort, hapa Chake Chake.
Msimamizi wa jengo hilo, Bwana Khamis Ali, anaifahamu vyema historia ya Mapinduzi. Si kweli kama Mapinduzi yamefanywa na watu wa Unguja pekee. Kihistoria, visiwa hivi vina maingiliano mkubwa kabla ya 1964 na walishaingilia kifamilia maana wote walishachanganya damu. Hivyo huwezi kumbagua yupi Mpemba na yupi Muunguja na hakuna wa kubishia suala hilo. Hivyo mapinduzi ni ya watu wote, anasema Bwana Khamis.
Bwana Salim Seif, ambaye pia ni mfanyakazi wa Idara hiyo ya Makumbusho, anakumbusha kuwa Waziri wa Elimu wa mwanzo katika Serikali ya Mapinduzi ni Ali Sultan Issa, ambaye pamoja na kundi kubwa la vijana walihama chama cha Hizbu na kuunda Umma Party, ambayo baadaye iliungana na Afro Shirazi Party kwenye Mapinduzi. Ali Sultan ni mzaliwa wa Pemba halisi kutoka Wete.
Watu wengi wanashindwa kufahamu dhana ya Mapinduzi. Wanajua kuwa ni yale mapigano na mauaji tu ndio Mapinduzi. Lakini wanasahau kuwa Mapinduzi yalikua ni mipango ya siri yenye mazungumzo nyeti na ilikua ni mipango mirefu. Kwa mantiki hiyo, kuna wengi walioshiriki kwa namna moja ama nyengine na ndio maana mara baada ya kupatikana kwa serikali, Bwana Ali Sultan akakabidhiwa uwaziri wa elimu, anasema Bwana Salim Seif.
Lakini hata kuelekea tukio lenyewe la Mapinduzi, mingoni mambo yanayokumbukwa sana na wazee wa Kipemba ni kile wakiitacho Kafya (inayotokana na neno la Kiingereza curfew).
Mwandishi wa makala haya alimuonesha Bwana Salim Seif picha ya kile kinachoitwa Kamati ya Watu 14 ambao wanasadikiwa ndio waliopindua, na ambamo ndani yake hamuna hata mtu mmoja wa Pemba, ikiwa ni moja ya hoja ya ukosefu wa ushiriki wa Wapemba kwenye Mapinduzi ya 1964.
Ni kweli kuna watu hawa 14 wanaoambiwa kuwa walipindua, ila kiukweli na usahihi hakuna nchi iliyopinduliwa na watu 14. Ni jambo ambalo haliwezekani kabisa. Isipokuwa kulikuwa na watu wengi sana walioshiriki katika mapambano hayo wakiwemo na Wapemba, anasema Bwana Salim Seif.
Bwana huyu wa Idara ya Makumbusho Pemba si mtu mzima pekee mwenye hoja ya kwamba Wapemba walishiriki kufanikisha Mapinduzi ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima cha Tanzania (Alliance for Tanzanian Farmers AFP), Bwana Said Soud, anakumbuka kuwa Mzee Karume alifanya mkutano katika eneo la Machomane, ambapo aliwajuulisha Wapemba kuwa chama chake kitafanya Mapinduzi.
Mzee Karume alikuwa ana kawaida ya kuja Pemba na akifikia Wawi kwa marafiki zake wa karibu na hawa ndio waliokua wakipanga pamoja kwa sababu walihangaika sana kutafuta uhuru kupitia kura lakini hawakuupata, anasema Bwana Said Soud.
Miongoni mwa marafiki wakubwa wa Mzee Karume ambao walijitolea nyumba, mali na hali zao kwa mapambano ya kudai uhuru kupitia ASP ni pamoja na Bi Bitsiin, Sheikh Ali bin Juma (baba wa aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar na baadaye Makamu wa Rais wa Tanzania, Marehemu Dk. Omar Ali Juma), Mzee Khamis Bin Hamad, Nassor bin Ismail, Rashid bin Mohamed (baba wa mbunge wa Wawi, Bwana Hamad Rashid Mohamed) pamoja na Mzee Haji bin Kombo (baba wa mbunge wa Chake Chake, Bwana Mussa Haji Kombo).
Wazee hawa walikuwa marafiki wa karibu sana wa Mzee Karume na walikuwa wanasikizana kwa kila kitu. Wakati vuguvugu la mapinduzi lilipotaka kuanza, wazee hawa ndio waliokuwa wakipanga naye. Sasa iweje iambiwe Pemba hawakushiriki katika Mapinduzi hayo? Anauliza Bwana Said Soud.
Mwenyekiti huyu wa chama cha upinzani ana kumbukumbu sio tu ya ushiriki wa Pemba katika upangaji wa Mapinduzi, bali pia katika tukio lenyewe la kupindua. Anasema yeye alilelewa na Mzee Khamis bin Hemed, ambaye alikuwa mwanachama na mwanaharakati wa chama cha ASP. Siku moja, wakati wakiwa wanakula chakula cha usiku, Mzee Khamis alimwambia mwanawe:
Kesho utasafiri kwenda Unguja. Nitakupa kadi yangu ya Afro-Shirazi ambayo itakua ndio utambulisho wako. Utafikia Miembeni, halafu utakuja kuchukuliwa mwende mukavamie kwa ajili ya kupindua serikali ya kikoloni.
Na kwa mujibu wa Bwana Said Soud ni kweli kwamba alikwenda na kufanya kama alivyoagizwa na mzee wake huyo. Iweje Wapemba waambiwe hawajashiriki? Naye pia anauliza.
Mzee Mkadara ambaye sasa ni mtu mzima wa miaka 90 aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama cha ASP na baadaye Chama cha Mapinduzi. Mzee huyu ambaye anafahamika kwa msimamo wake usioyumba wa kuiunga mkono CCM, hata wakati ambapo watu wengi kisiwani Pemba walipoacha kufanya hivyo, anasema kwamba hakuna mtu yeyote anayethubutu kuwabagua Wapemba kwenye hili la Mapinduzi, kwani wameshiriki.
Naye pia ana kumbukumbu za Wapemba wengi ambao walishiriki kwenye tukio lenyewe la Mapinduzi na wengine kupoteza maisha yao.
Mmoja wao ni Mzee Haji. Huyu alizaliwa na akaishi Micheweni, alikokuwa askari. Kipindi cha Mapinduzi alishiriki kikamilifu katika kugawa silaha kwa wapinduaji ili kuhakikisha nchi inakombolewa. Wanaosema kuwa sisi hatukushiriki, hao ni watoto wadogo ambao hawajui kitu na hawajui wapi tunapotoka, anasema Mzee Mkadara.
Halafu kuna na Field Marshal John Okelli ambaye ingawa hana damu ya Kipemba lakini alitokea Pemba kwenda Unguja kupindua. Haielekei kwamba ni yeye peke yake aliyetoka Pemba kwenda Unguja kwashughuli hiyo ya kupindua bila ya kuwa na washirika wake.
[h=1][/h]khelef / 7 days ago

Vijana wa Umoja wa Vijana wa ASP kisiwani Pemba.